Hakuna mahusiano hapo kwani kila nchi inaruhusiwa kuonesha baadhi ya mechi za kombe la Dunia kupitia television ya taifa, ispokuwa kwa baadhi ya mechi
Kwa kifupi ni kwamba kuanzia mwaka 2010,2014,2018 na miaka ya nyuma pia kombe la Dunia tumekuwa tukiangalia kupitia television ya taifa, tangu enzi za TVT
Ata mwaka 2018 Azam hakuonesha kombe la Dunia kutokana na Mambo ya haki miliki za DStv na bado wale wasiokuwa na DSTV waliangalia baadhi ya mechi TBC au television ya taifa ya Kenya/Uganda
Azam hana haja ya kuingilia mlango wa uwani kwani huo ni utaratibu wa miaka yote, na sio kwamba TBC itaonesha mechi zote, lahasha kuna baadhi ya game itakubidi tu utafute DStv ilipo
Na ata kama akifanya hivo bado sioni kama atapata faida yoyote ile na sioni kama atampa hasara yoyote ile DStv, Kwa sababu DStv utaangalia mechi zote na kama hiyo haitoshi utaangalia Kwa quality ya juu sana tofauti na ule uchafu wa TBC
Kwahiyo Kwa uelewa wangu Mie sidhani kama kuna uhusiano wowote ule Kati ya Azam na TBC kuonesha kombe la Dunia kwani miaka yote inakuwa hivo sasa Sijui kipi kimebadirika hadi uhisi kuwa Azam ana mkono wake