Elections 2010 TBC Live TARIME leo

Elections 2010 TBC Live TARIME leo

kuna mzee anauliza swali hapa....anasoma....kwamba watu wanaokula hela za maendeleo zinazokuja watawadhibitije?

CHADEMA wanajibu kuwa wagombewa wao ni makini...na wanakazi ya kuhakikisha kuwa kilicholengwa kwa wananchi kinatumika kwa ajili ya wananchi na atakayeenda kinyume anaondolewa mara moja kwa ngguvu ya umma

NCCR mageuzi: anasemakuwa lazima kuwa na wataalam wa mambo ya pesa, kuhakikisha pesa zinaenda vijijini,

UDP: Mchungaji anasema kuwa atasimamia sawa sawa kwa vile ni mchungaji....atatumia sheria KALI...yeyote aliyefilisi mali ya tarime naye atafilisiwa

CUF: Anadai kuwa akiwa mbunge alisimamia halmashauri kwa busara.....alihakikisha kuwa hakuna mkono wa mtu unapita..akichaguliwa ataendelea kusimamia...
 
Chadema wanajitahidi kwa kunukuu ilaniinaonyesha si maneno ya kulipuka ni mipango ya chama
 
Kaizer shukrani sana kwa kutuletea habari hizi ,endelea tafadhali
 
Kuna mama mmoja anauliza kero , amani hakuna, wanawake wanadhalilisshwa, vijana hawakai ndani kwa vile wamechafuka.....(mtangazaji anasema kuwa llimeshazungumzwa mwanzoni, watu wanagombea kuuliza maswali)

mama mwingine anauliza, je wakipewa kura, kanda maalum iliyopo tarime inasumbua sana...watafanya nn?

CHADEMA wamesema kuwa watasimamia kanda maalum kwamba inanyanyasa wananchi...wamejipanga, kuwe na tathimini kwa kutumia wananchi ipelekwe hoja binafsi bungeni...kanda maalum iondolewe (hivi kumbe hawaipendi eeh?)

Kuna diwani anauliza: kuhusu maji ya sumu kuna kamati ziliundwa hazijafanya kazi kuhusu m..aji ya sumu kwa walioathirika...

Mchungaji anajibu kuwa sio mgeni wa kudai haki za watu....sheria za fidia zipo ataenda mahakamani

CUF -anasema kuwa alikuwa mbunge na aliliwakilisha bungeni....(majibu ya ile tume yako wapi?)
 
sasa muda wa summary

Wa NCCR anasema kuibua miradi kutoka chini, aipeleke juu,

Wa Chadema anasimama nakushangiliwa anaomba kwamba 2010 wapige kura za kimkakati wachague chadema, wapige kura kwa diwani mbunge na raisi wa chadema..........

Wa UDP mchungaji yupo karibu san na wananch kuliko wanasiasa...anasema wasiipe UDP wampe mchungaji...anaomba kura za ndiyo

CUF: anasema walimpa kwa muda mfupi, kwa miak 5 miradi waliyoanzisha ataisimamia....

so kipindi kimeishia hapo....ha sasa huyi wa CHADEMA NA CUF mbona hawapeani mikono wajameni:confused2::confused2:
 
Kaizer shukrani sana kwa kutuletea habari hizi ,endelea tafadhali


Naona kipindi kimeisha but thats my contirbution kwa leo kwa wale ambao hawajaweza kuona kipindi hiki live leo. nadhani wapo walioweza kurekodi huenda wakatuwekea zome clips hapa kuweza kupata ile feeling hasa ilikuwaje

CCM kutoweka wagombea wao wanafanya kosa kubwakwa maoni yangu maana hapa ndio ingekuwa nafasi nzuri ya kuzidiana kisera,

Ila pia sijapenda uulizaji huu wa maswali wa TBC nadhani ile issue ya ubungo bado inawatafuna tafuna nod wamebadili strategy... maswali ingebidi yawe specific kwa kila mgombea bana..
 
Hii kipindi imekuwa muda mfupi. Halafu jamaa wa TBC alikuwa anambania Mwita .Nilichojifunza ni kwamba, watu wa Mara haswa Tarime sio wanafiki
 
Mbona wote nimeona na kusikia wakizungumza kiswahilikurya? kumbe tatizo la lafudhi ni la kila lugha?:becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky:
 
Hapa aliharibu sana tu, kwa nini hawa waamini wagombea wao?
Kwa kuwa hajiamini na hamuamini mgombea wake wa urais; Anaona heri nusu shari kuliko shari Kamili hataki wagombea wa ubunge waonekane bora kuliko Rais wake
 
Ilani ya CHADEMA HAISEMI elimu ni bure hadi form 6.

Wewe acha kuchanganya mambo bana. Wote tunasoma Ilani hizo hizo.

CHADEMA imesema elimu bure kuanzia chekechea mpaka kidato cha sita.

CUF wamesema elimu bure kuanzia chini mpaka Chuo Kikuu.

Soma tena hizo Ilani za vyama katika kipengele cha elimu.
 
Hapa aliharibu sana tu, kwa nini hawa waamini wagombea wao?

Mkuu, sio tu kwamba hawaamini wagombea wa CCM, bali kawatukana tusi kubwa kuwa ni mabumbumbu wote na hawajui kujieleza. Inatia hasira kweli kuona kuwa wote wametumbukizwa kwenye tenga moja na kuzibwa midomo, ilhali kuna baadhi ni wakweli na wanathamini maendeleo ya Taifa letu na ingelikuwa fursa kubwa kwao kushiriki kwenye mdahalo.
 
Kama vile mlogwa vile!!! yaani...

Mkuu Kasheshe,

Ndugu zako CCM wanakimbia Mdahalo kwa kuwa hata haieleweki kwamba wana sera gani. Umeona kile alichokisema Sitta kwenye hotuba yake ya kuzindua Kampeni Jimboni kwake? Anasema atasomesha watoto yatima 40, je jimbo lake lina watoto yatima 40 tu? Kama wapo zaidi ya hao? What about wale ambao wazazi wao hawana uwezo? Atatumia kigezo gani kuwapata hao 40 ambao atawasomesha? Hapo ndio ametatua tatizo la elimu kwa jimbo lake?

Mara ameanza kukandia habari za ufisadi, yeye alikuwa wa kwanza ku-doubt documents za hoja ya EPA alipopelekewa na Dr. Slaa, alisema vithibitisho/ushahidi ulioambatanishwa ana mashaka ni wa kugushi. Tangu alivyopeleka Polisi ili wakachunguze hakuwahi kutoa taarifa. Leo hii anasema watu wakiongelea ufisadi wa CCM na Kikwete, eti wanatumia lugha ya matusi. Amesahau kwamba yeye ndo alikuwa anajiita kiboko ya mafisadi mara sijui mpambanaji wa ufisadi mara sijui Kamanda, kwa hiyo alikuwa anajitukana mwenyewe wakati huo?

Sasa mtu kama huyo mpeleke kwenye Mdahalo halafu ifike wakati wa maswali uone jinsi anavyojikanyaga. Pamoja na kwamba huwa unawaponda wapinzani lakini bado tunarudi pale pale CCM kukimbia midahalo imeonyesha jinsi ambavyo hawana uwezo wa kujibu maswali ya wananchi. Wanakimbilia kwenye kuwadanganya baada ya hapo hakuna maswali wala nini.

JK alipokuwa Kigamboni aliulizwa swali la kuiendeleza Kigamboni, aliruka kimanga, kwamba hilo linaweza kujibiwa na Diwani wa Kigamboni ambaye hayupo eti kaenda kugombea Ubunge kwao Mtwara. Hizo ndio Kampeni za CCM hata rais anakimbia maswali ambayo maamuzi yake yana baraka za Baraza la Mawaziri ambalo yeye ni Mwenyekiti. Kama siyo hila ni nini?

Ninakubali nitabaki kama nimerogwa, lakini siwezi kushabikia ujinga wa CCM ambao unatupeleka kaburini. Already wananchi wanalia kwa kukosa ardhi, na Kikwete hana majibu anasema atabembeleza wawekezaji ili wakubali kuuza tena ardhi ile ile waliyonunua kwa bei chee. Hapo hapo anahamisha wakazi wa Kigamboni ili ardhi ya Kigamboni awape wawekezaji. Kwanini serikali inakuwa ndo wakala wa wawekezaji? Kwanini wawekezaji wenyewe wasiongee na wenye nyumba zao? BS!
 
Wana JF,

Tatizo la chama hiki(CCM) ni kuto jua alama za nyakati. uanzishapo kitu then unafika mahali hujui uendako ni mbaya sana, kura za maoni wakadhini ndio itakuwa bora na kuondoa zogo baina ya wanachama na kumbe ndio mwaongeza zogo lisilo zimika hata kwa aina gani ya maji,

Mpaka sasa CCM hakija toa tamko rasmi kwanini wagombea majimboni hawaruhusiwi kuingia kwa mdahalo??? eg "Lusinde mgombe ubunge CCM Mtera anajitamba kuwa yeye ndie mwanume waliopita wote sio wanaume sasa hii kauli kweli inaashiri hawa ndio vijana wa leo jamani hii inashusha hadhi ya UVCCM kabisa na kupoteza imani kwa vijana wajao kati uongozi wa UVCCM"

Je chama chaendeshwa ki ubabe au? nini maana ya democrasia?? na hii ni tatizo kubwa kwa CCM kwani wapiga kura wao wengi ni vijana na vijana wengi wamejikita kwa UVCCM na hao vijani baadhi yao walisha rubuniwa na njaaaa means wameisha pewa mrungula ili kuwa rubuni wenzao na hapo ndipo chanzo kikubwa kwa CCM kugawanyika kwani hawana uhakika wa UVCCM huko waliko kama wanaunga mkono wabunge walio teuliwa kwa kura za maoni CCM au raah?

Makosa ya viongozi wa juu wanajaribu kuyaepusha ili wasionekane walichemka esp Katibu mkuu CCM makamba?? ila najua ukombozi wa CCM unakuja very sooon hawawezi zui mvua kunyesha kwa viongozi walipo, kwani chama si chao bali ni chawananchi na sio kuwa wao ndio watakuwa hapo CCM milele.

 
Back
Top Bottom