Kama vile mlogwa vile!!! yaani...
Mkuu Kasheshe,
Ndugu zako CCM wanakimbia Mdahalo kwa kuwa hata haieleweki kwamba wana sera gani. Umeona kile alichokisema Sitta kwenye hotuba yake ya kuzindua Kampeni Jimboni kwake? Anasema atasomesha watoto yatima 40, je jimbo lake lina watoto yatima 40 tu? Kama wapo zaidi ya hao? What about wale ambao wazazi wao hawana uwezo? Atatumia kigezo gani kuwapata hao 40 ambao atawasomesha? Hapo ndio ametatua tatizo la elimu kwa jimbo lake?
Mara ameanza kukandia habari za ufisadi, yeye alikuwa wa kwanza ku-doubt documents za hoja ya EPA alipopelekewa na Dr. Slaa, alisema vithibitisho/ushahidi ulioambatanishwa ana mashaka ni wa kugushi. Tangu alivyopeleka Polisi ili wakachunguze hakuwahi kutoa taarifa. Leo hii anasema watu wakiongelea ufisadi wa CCM na Kikwete, eti wanatumia lugha ya matusi. Amesahau kwamba yeye ndo alikuwa anajiita kiboko ya mafisadi mara sijui mpambanaji wa ufisadi mara sijui Kamanda, kwa hiyo alikuwa anajitukana mwenyewe wakati huo?
Sasa mtu kama huyo mpeleke kwenye Mdahalo halafu ifike wakati wa maswali uone jinsi anavyojikanyaga. Pamoja na kwamba huwa unawaponda wapinzani lakini bado tunarudi pale pale CCM kukimbia midahalo imeonyesha jinsi ambavyo hawana uwezo wa kujibu maswali ya wananchi. Wanakimbilia kwenye kuwadanganya baada ya hapo hakuna maswali wala nini.
JK alipokuwa Kigamboni aliulizwa swali la kuiendeleza Kigamboni, aliruka kimanga, kwamba hilo linaweza kujibiwa na Diwani wa Kigamboni ambaye hayupo eti kaenda kugombea Ubunge kwao Mtwara. Hizo ndio Kampeni za CCM hata rais anakimbia maswali ambayo maamuzi yake yana baraka za Baraza la Mawaziri ambalo yeye ni Mwenyekiti. Kama siyo hila ni nini?
Ninakubali nitabaki kama nimerogwa, lakini siwezi kushabikia ujinga wa CCM ambao unatupeleka kaburini. Already wananchi wanalia kwa kukosa ardhi, na Kikwete hana majibu anasema atabembeleza wawekezaji ili wakubali kuuza tena ardhi ile ile waliyonunua kwa bei chee. Hapo hapo anahamisha wakazi wa Kigamboni ili ardhi ya Kigamboni awape wawekezaji. Kwanini serikali inakuwa ndo wakala wa wawekezaji? Kwanini wawekezaji wenyewe wasiongee na wenye nyumba zao? BS!