TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

hahahaa...wenyewe wanakwambia wana kitu kinaitwa "weledi"...sijui ni mchele wa wapi huu......mtu yeyote akisemwa ana hiki kitu hua ana peform below international standards...sijui kwanini....
 
hamna umakini wa kazi nmafanyafanya tu inaboa
ubuniffu zero inaboa
kurudia rudia vipindi inaboa
ongezeni production plz mbona ragmhis tu jmn!
[emoji32]
 
TBC CCM Toka asubuhi mpaka jioni Vipindi vya kumsifu mtukufu tu ujingaaaa mtupu
 
Acheni kuitumia tbc na propaganda za ccm channel ten si mmeinunua itumieni kwa matumizi ya ccm Kama gazeti la Uhuru tbc iachane huru Kama ilivyo KBC

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tbc ni television ambayo haifai kuangaliwa na Yeyote ambaye anajitambua, ina upendeleo dhahiri shahili, ni kama tv ya ccm tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kujitambua kupi? Kwanini umseeme kila mtu eti kwa yeyote? Kwahio kila moja afungwe na itikadi za kisiasa hapana jisemee mwenyewe Mimi naangalia vipindi vya elimu mbalimbali ukizama kiitikadi Chanel zote wamiliki wanaweza kua wanachama wa vyama mbalimbali jee tusiangalie eti sabababu za itikadi zao hatuwezi fika ndugu yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuombe radhi kaka kina Nshomile hatufanyi kazi TBC.... Sisi ni watu wa CNN....ALJAZEERA. N.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TBC bhana kuna siku kulikuwa na event moja hivi Dodoma chuo cha mipango iliyoandaliwa na TBC, kuhusu mambo ya viwanda.
Nilikuwa mmoja wa participants wa hiyo event, sasa wale main characters wakaanza kujitambulisha, mzee mmoja hivi alinifata akaniomba nimtajie spelling za jina la mmoja wa wahusika wakuu wa hiyo event akidai yeye hakuskia vizuri.
Huyo mzee alikuwa ananuka pombe saana na niliskia ni mmoja wa editors wa TBC, halafu anatetemeka hatari yani sio poa. Sasa kwa aina hiyo ya wafanyakazi TBC haiwez fika popote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri iweje changamoto ziishe unazodai wewe?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Channel mpya ya Safari Channel ilipoanza ilionekana kama chaneli tishio kwa sababu watu wengi sana wanapenda kuangalia wanyama na matukio ya utamaduni wetu.Watu wengi awali walikuwa waking alia chaneli za wanyama za nje lakini baada ya kufunguliwa hii chaneli ya kwetu watu walihamia nyumbani.Baada ya muda mfupi tayari waandaji wa vipindi vya chaneli hii wameanza kuharibu kwa kasi ya ajabu na tayari watu wameanza kurudi kwenye chaneli zao za nje.Vipindi vingi vya Safari Chaneli vinarudiwa rudiwa mno hadi inakuwa chukuzo.Kuna makabila mengi Tanzania ambayo yote yana utamaduni wao lakini nafasi hayapewi.Mikanda ya wanyama iko mingi na mizuri mno lakini yote haioneshwi kamwe.Waandaji wanashindwa hata kumuenzi mzungu alietengeneza mkanda mashuhuri wa wanyama uliojulikana kwa jina la SERENGETI SHALL NEVER DIE.Huyu mzungu simkumbuki jina lakini katika harakati zake za kupiga picha za wanyama katika mbuga ya Serengeti kwa kutumia helicopter yake binafsi alipata ajali baada ya ndege kugongwa na mapopo na kuanguka na yeye alifarika dunia.Baada ya ndugu zake kufika toka Ulaya waliamua azikwe Tanzania na kujengewa mnara wa kumbukumbu pale pale alipoangukia na ndege yake.Mtoto wake mkubwa katika kutoa neno kwa serikali ya Tanzania alitamka neno la ajabu na la kishujaa mno.Nanukuu alivyosema mtoto huyo, " Baba amekufa lakini Serengeti haitakufa.Alichukua mikoba ya baba
na kumalizia kazi ya kupiga picha wanyama.Filamu yake aliita SERENGETI SHALL NOT DIE!!.Ni picha iliovutia mno watazamaji kipindi kile.Waandaji wa vipindi vya Safari Chaneli sidhani hata kama wanafahamu kumbukumbu hii muhimu na si ajabu hata nakala ya ya picha hawana.Ni aibu kufuta kumbukumbu ya jinsi hii.Nawasihi itafuteni ili vijana wa sasa waweze kujifunza kutoka kwenye mkanda huo wa kusisimua.Kwa sasa watu wamechoka mno navipindi vya kurudia yale yale kila siku.
 
Hii ni wengi hatuifuatilii japo baadhi ya ving'amuzi wamejitahidi kuondo local channel ili tuitizame ila bado

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyambona Masamba apewe kazi nyingine sio usomaji wa habari za kimataifa kwa sababu sauti yake inatokea puani na haisikiki vizuri hadi inakuwa kero na mateso matupu kumsikiliza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa TBC1 tuliambiwa mnakamilisha kufunga mitambo ya nguvu ili picha ziwe angavu yaani HD vipi lini hiyo project inakamilika...maana picha ubora unakwaza wanandugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aidha nashauri mfikirie kufanya uwekezaji mkubwa wa studio sets za TV nikishauri mkajifunze KBC au CITIZEN TV Kenya mpate designer wa studio za kisasa kama za wale wenzetu...studio za sasa zinapwaya sana hasa kwa mtindo wenu wa multiple hosting ya vipindi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…