Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Inabidi wajitathimin wao wenyewe TBC vipindi vyao vimekosa ubinifu. Watafute mkurungezi wa vipindi anae endana na wakati, waajili vijana wabunifu katika kuandaa vipindi.
 
Tatizo la wafanyakazi wa TBC hawatafuti habari. Ukiwambia njoo huku vijijini kuna habari wanakwambia type 500,000/=. Je, wanalipwa mshahara kwa lipi kama hatafuti taarifa vijijini. Hufuatana tu na viongozi wakubwa. Nani ataandika habari za wakulima kama siyo TBC. Vyombo vingine vimejikita kutoa taarifa zinazogusa maisha ya kila siku ya Mtanzania bila hata kuomba fedha kwa watoa taarifa. Mfano star TV watumishi wake wanajituma hasa.
 
Wakati Alipo kuepo Tido Muhando Aliludisha Iman Kwawatazamaji Lkn Alipo Ondoka Wakaludi Ktk Mfumo Wao Kama Chombo Cha Kisiasa Mimi Kwangu Imekua Nikama Mwiko Kutadhama Chombo Icho Mpaka Watakapo Jirekebisha
Una point lakini Kiswahili umeharibu sana. Aliludisha=alirudisha; wakaludi=wakarudi; sitadhami=sitazami; icho =hicho. Furahi kwani hauko peke yako. Hili ni tatizo la nchi nzima!
 
Una point lakini Kiswahili umeharibu sana. Aliludisha=alirudisha; wakaludi=wakarudi; sitadhami=sitazami; icho =hicho. Furahi kwani hauko peke yako. Hili ni tatizo la nchi nzima!
[emoji3][emoji3][emoji3]uchokozi huo mkuu
 
TBC inakera sana....wanakipindi cha cha Naibu waziri wa Nishati na Madini,kikiisha kinakuja cha TASSAF,kikitoka kinarudi cha Naibu Waziri,kikiisha TASSAF.

Yaani msoma habari akisubiri picha mpaka unamuonea huruma.....mi nadhani kifungwe kwa mwaka mmoja kwanza.
 
mi naona tatizo pia katka vipindi, bado vya kizamani, bongo flava zinapigwa tukishalala, vipindi vya bunge vinaeditiwa ili usiwaskie wapinzani, pia ni usiku, ndio maana siipendagi siku hizi, nikiiangaliaga huwa nalala mapema, nahisi macho yangu yanaanza kuwa na alegi
 
Nyie mnapotoshwa maboya,wenzenu watakuwa wamekaa ili kujiandikia mzigo WA Xmas na Nyie kwa kuwaza haraka haraka mmedhani wanadiscuss performance.
Ule ulikuwa mkesha mahsusi ukienda kucheck muamala WA Oc ndio utaelewa walikuwa wanajadili nini
Nakubaliana na wewe kwa 100% tatizo la TBC hakuna asiyelijuwa Dr Riobaamshauri Magufuli awape pesa ccm waanzishe tv yao ya propaganda zao na Tbc iachwe huru iingie kwenye ushindani wa kibiashara, mimi hilo litv la hovyo nilikuwa naangaliaga bunge tu lakini tangu wameondoa bunge sijui kinachoendelea Tbc.
 
Sasa Mnajiloga halafu mnashangaa kudorora, mtu analeta tangazo la kumbukumbu lirushe tarehe na muda fulani sasa ninyi mnaonyesha harusi live, mkiulizwa mnadai kulikua na dharura mtarusha keshokutwa yake, sitakagi hata kuangahia tbc
 
Itakuaje ikiwa habari nyingi zinazotangazwa zina kuwa na upendeleo, kama habari zinakuwa na hali ya vyama vya upinzani haitangazwi.... sasa hayo maendeleo mnayataka ya aina gani?
 
Watanzania tumechoshwa na habari UCHWARA za kuwafagilia MACCM chama cha wahuni, majangili, Wakwapuzi, mafisadi, wezi, watoa na wapokea rushwa na wahuni.
 
Uonngozi wa juu wa TBC na wafanyakazi wengine wa kituo hicho usiku wa kuamkia leo wamefanya kikao cha dharura kuangalia sababu za kudorora kwa kituo hicho kikubwa cha TV ambacho kimemalizika saa 11 alfajiri.

Pamoja na mengine kitu kilichoonesha kuwaumiza kichwa zaidi ni jinsi gani kituo kikubwa kama hicho kinachopata ruzuku kubwa kutoka serikalini kinakuwa na ratings za mwisho huku kikizidiwa na vituo ambavyo havina hata miaka mitano hewani.

Mkurugenzi amesisitiza sana na kuwaomba wafanyakazi wa TBC kama ikitokea rais anapiga tena simu kwenye kituo chochote cha TV basi iwe TBC na ikiwa anatuma kadi ya salamu basi iwe TBC.
UBAGUZI NA UPENDELEO BILA KUFUATA WELEDI WA KUFANYA KAZI KAMA SHIRIKA NA MALI YA WATANZANIA WOTE, ndo kinacho itesa TBC
 
Kama muda wote huo walikua wakijadiliana ili kujua tatizo liko wapi, basis wameshashindwa. Maana tatizo wanalijua lakini wanaliogopa.
 
Back
Top Bottom