TBC wanaandika Jenerali Musuguri alizaliwa 1920, Mkuu wa Majeshi ameandika katika taarifa rasmi, kwamba Musuguri alizaliwa 1925. TBC mjirekebishe

TBC wanaandika Jenerali Musuguri alizaliwa 1920, Mkuu wa Majeshi ameandika katika taarifa rasmi, kwamba Musuguri alizaliwa 1925. TBC mjirekebishe

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Wahariri wa TBC siwaelewi, wana access ya Mkuu wa Majeshi, Msemaji wa Jeshi, lakini bado wanakosea. Hata katika taarifa ya habari ya saa moja usiku wa leo, habari inahusu Mkoa wa Mwanza, caption imeandikwa Kigoma.

Anyway, kwa tuliosoma Kyuba, pale palipoandikwa marehemu "ameacha familia" tumeelewa kwamba huko katika sekta ya familia pia alitumikia taifa vizuri. Makamanda wote ni waumini wa moja kati ya "WWW"
Screenshot_20241029-201654.jpg
 
Hii ni changamoto ya jumla ya kizazi hiki, umakini umepungua katika nyanja zote nchini, kuanzia raia wa kawaida hadi viongozi
Zaidi sana kukosa weledi kunawafanya watu kuwa maarufu.
 
Hata magazeti yao hivyo hivyo makosa kibao yaani wahariri wa hovyo sana
Kila wakiandika, makosa ya kijinga sana unaona tena front page kabisa
Tumewazoea maana hata wa kuwakosoa ni wale wale hawaoni makosa kabisa kwa sababu aidha kubebana makazini au mbumbumbu tu
 
Mleta uzi umeanza lini kumfuatilia huyu Jenerali ?
Isijekuwa umeanza kumfahamu leo.
 
Wahariri wa TBC siwaelewi, wana access ya Mkuu wa Majeshi, Msemaji wa Jeshi, lakini bado wanakosea. Hata katika taarifa ya habari ya saa moja usiku wa leo, habari inahusu Mkoa wa Mwanza, caption imeandikwa Kigoma.

Anyway, kwa tuliosoma Kyuba, pale palipoandikwa marehemu "ameacha familia" tumeelewa kwamba huko katika sekta ya familia pia alitumikia taifa vizuri. Makamanda wote ni waumini wa moja kati ya "WWW"
View attachment 3138564
Kwa taarifa yako hakuna hata mmoja aliyesema kweli kwenye hilo. Kuanzia marehemu, mkuu wa majeshi hadi hao TBC. Wote kila mmoja ametoa tarehe ya kukadiria na sio tarehe ya kweli.
 
Nilitaka kusema hili pia, what if mkuu wa majeshi ndio kakosea....
Si ndio hapo sasa. Nijuavyo mimi kwa miaka hiyo na hasa kwa waliozaliwa huko vijijini, ilikuwa ni nadra sana watu kujua tarehe zao halisi za kuzaliwa. Sana sana watu walikuwa wanakadiriwa miaka kutokana na kutaja matukio yaliyokuwa karibu na simulizi zao au wazazi wao.
 
Kazi za kupeana bila kuzingatia weledi na taaluma haya ndio matokeo yake
Hauko sahihi .

Huko nyuma fani zote ziliajiri hata watu wasiosoma kabisa na waliweza kupanda vyeo kihalali kabisa. Zamani hakukuwa na bodi mbalimbali za kitaaluma tena zenye meno kama sasa.

Nakumbuka zamani mtu akimaliza shule kijijini anakuja mjini kutafuta kazi na anapata kazi.

Ndio maana elimu za zamani nyingi ni za kujiendeleza, wako watu waliingia serikalini wakiwa form iv lakini wamesoma wakiwa humo humo na leo ni madokta wa PhD.

Kuhusu tofauti ya tarehe za kuzaliwa kwa watumishi wengi wa zamani walirudisha umri nyuma sasa unakuta nyaraka tofauti tofauti zinazowahusu waliandika tarehe tofauti za kuzaliwa hawakuwa wanakumbuka kuharmonise.
 
Back
Top Bottom