TBC wanaandika Jenerali Musuguri alizaliwa 1920, Mkuu wa Majeshi ameandika katika taarifa rasmi, kwamba Musuguri alizaliwa 1925. TBC mjirekebishe

TBC wanaandika Jenerali Musuguri alizaliwa 1920, Mkuu wa Majeshi ameandika katika taarifa rasmi, kwamba Musuguri alizaliwa 1925. TBC mjirekebishe

Hii TBC ya sasa wameajiri waandishi na watangazaji wenye ufahamu mdogo maadamu wanaona wamepitia vyuo na wana vyeti, ila hawana weledi mkubwa kwa taaluma hiyo
 
Viwango vimeshuka, kila sehemu. Sijui tutafikia kilele cha kushuka lini, ili tuanze kujenga upya. Tusipo bahatika, tutabaki huko huko chini, mithili ya Haiti!
Hatari sana.
Halafu unakuta mpaka Waziri wa Habari anasoma utumbo huo
Kweli hatuna tofauti na Haiti ambao wao wamejichagulia pia maisha kama yetu
 
Si ajabu na si mara ya kwanza kusikia taarifa za mtu aliyewahi kuwa mtumishi serikalini kutofautiana na taarifa za watu wengine. Alichofanya CDF ni kucheki jalada la mstaafu na kilichomo; hakuhitaji kuuliza mtu mwingine kupata historia ya utumishi wa marehemu.
Lakini mwaka 2020 alifanyiwa 'birthday' nyumbani kwake akidaiwa kufikisha miaka 100..!
 
Wahariri wa TBC siwaelewi, wana access ya Mkuu wa Majeshi, Msemaji wa Jeshi, lakini bado wanakosea. Hata katika taarifa ya habari ya saa moja usiku wa leo, habari inahusu Mkoa wa Mwanza, caption imeandikwa Kigoma.

Anyway, kwa tuliosoma Kyuba, pale palipoandikwa marehemu "ameacha familia" tumeelewa kwamba huko katika sekta ya familia pia alitumikia taifa vizuri. Makamanda wote ni waumini wa moja kati ya "WWW"
View attachment 3138564
Kuna siku Makamu wa Rais, Dkt Mpango akiwa kwenye sherehe ya Siku ya Misitu Kilimanjaro, waliandika watu bilioni 10 Afrika wanatumia mkaa, nilishangaa sana.
Wakati duniani watu ni bilioni 8.2
Hapo TBC sema kazi ni za kujuana sana.
 
Wahariri wa TBC siwaelewi, wana access ya Mkuu wa Majeshi, Msemaji wa Jeshi, lakini bado wanakosea. Hata katika taarifa ya habari ya saa moja usiku wa leo, habari inahusu Mkoa wa Mwanza, caption imeandikwa Kigoma.

Anyway, kwa tuliosoma Kyuba, pale palipoandikwa marehemu "ameacha familia" tumeelewa kwamba huko katika sekta ya familia pia alitumikia taifa vizuri. Makamanda wote ni waumini wa moja kati ya "WWW"
View attachment 3138564
Shida ni CDF kuzaliwa 1920
 
Hauko sahihi .

Huko nyuma fani zote ziliajiri hata watu wasiosoma kabisa na waliweza kupanda vyeo kihalali kabisa. Zamani hakukuwa na bodi mbalimbali za kitaaluma tena zenye meno kama sasa.

Nakumbuka zamani mtu akimaliza shule kijijini anakuja mjini kutafuta kazi na anapata kazi.

Ndio maana elimu za zamani nyingi ni za kujiendeleza, wako watu waliingia serikalini wakiwa form iv lakini wamesoma wakiwa humo humo na leo ni madokta wa PhD.

Kuhusu tofauti ya tarehe za kuzaliwa kwa watumishi wengi wa zamani walirudisha umri nyuma sasa unakuta nyaraka tofauti tofauti zinazowahusu waliandika tarehe tofauti za kuzaliwa hawakuwa wanakumbuka kuharmonise.
Wengi walipunguza umri
 
Aliwahi kuhojiwa yeye mwenyewe kipindi anasumbuliwa na miguu akasema kazaliwa 1920
 
Mleta mada acha tabia ya kuangalia TV (TBC1) iliyojaa watangazaji wasio na weledi (ndugu na jamaa wa maccm).
 
Wahariri wa TBC siwaelewi, wana access ya Mkuu wa Majeshi, Msemaji wa Jeshi, lakini bado wanakosea. Hata katika taarifa ya habari ya saa moja usiku wa leo, habari inahusu Mkoa wa Mwanza, caption imeandikwa Kigoma.

Anyway, kwa tuliosoma Kyuba, pale palipoandikwa marehemu "ameacha familia" tumeelewa kwamba huko katika sekta ya familia pia alitumikia taifa vizuri. Makamanda wote ni waumini wa moja kati ya "WWW"
View attachment 3138564
Marehemu atakuwa alizaliwa mara mbili
 
Back
Top Bottom