TBC watimuliwa mbio na CHADEMA baada ya kukata mara kwa mara matangazo ya uzinduzi wa kampeni Mbagala Zakhiem

TBC watimuliwa mbio na CHADEMA baada ya kukata mara kwa mara matangazo ya uzinduzi wa kampeni Mbagala Zakhiem

Status
Not open for further replies.
Wakuu wasalaam!

Nimeamua kuzima tv yangu na kuhamia kwenye online TVs baada ya kugundua kuwa TBC1 hawarushi matangazo ya uzinduzi moja kwa moja ziadi ya kukatisha matangazo pale Magufuli anapokosolewa jukwaani.

Kumbe ndiyo maana CHADEMA wameanza kampeni hizi kwa uwekezaji mdogo wa rasilimali.

Nyie pia mmegundua hilo?
 
Nilikuwa nina mashaka sana kama TBC wataweza kuvumilia na kuruhusu maneno machungu yatakapokuwa yanatolewa, bahati mbaya hofu yangu imekua kweli.

Wamesimama watu wawili kuzungumza wa kwanza alipoanza kumtuhumi JPM juu ya kutoongeza mishahara ya watumishi TBC waka-mute sauti wakaweka watangazaji wa studio, amesimama Lema alipoanza tu kuzungumzia juu ya Tume ya Uchaguzi wame-mute tena wameweka watangazaji wa studio.

Sasa kwa mwendo huu atakaposimama TL mwenyewe si na matangazo mtazima?

Mlipoamua kurusha kampeni ya chama cha upinzani mlitarajia kuna mapambio ya sifa? Ili mradi hakuna matusi au maneno ya uongo acheni tusikie sisi wenyewe tutapima pumba na mchele.

TBC, TBC, TBC hamuwezi jua come November bosi wenu anaweza kuwa huyu huyu mnayetaka kumnyima fursa ya kusikika kwa ukamilifu.
 
Naangalia TBC 1 hapa

1. Wanakatakata matangazo ya live kutoka Mbagala.
2. Wanaongea pointless watangazaji wao hapo studio.
3. Wanaonyesha vitoto vidogo vilivyopo mkutanoni.

My take: Chadema wasirudie kuiruhusu TBC 1 kurusha matangazo yao.
 
Uzinduzi tu upo hivi tena day one sijui baada ya siku 10 itakuwaje.
 
Hata wafanye figisu Awamu Hii Wanalo Wamelikoroga Kunywa Taurati.
 
TBC kwa maksudi kabisa wanahujumu matangazo ya moja kwa moja ya uzinduzi wa kampeni za urais wa CHADEMA. Mgombea ubunge wa Ilala na Lema walipoanza kushusha nondo tbc wakawa wanajifanya kuanza kujiongelesha ili watazamaji wasisikie kinachoongelewa.

Mgombea wa Ilala alianza kumwongelea Magufuli tbc wakajifanya wanajadili. Lema alipoanza kuelezea nchi inaongozwa kama gheto TBC wakahamisha tena.
 
Chadema watafute njia ingine ya kusambaza ujumbe wa mikutano yao.
 
Kinachofanyika ni kwamba muongeaji akianzankuigusa serikali na taasisi zake wao wanazima matangazo na watangazaji kujitia waongeaji na wachambuzi. Hili nililitegemea
Mkome kiranga, mnajifanya jorowe sio haya ndio mapigo yenyewe, na bado.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom