Nilikuwa nina mashaka sana kama TBC wataweza kuvumilia na kuruhusu maneno machungu yatakapokuwa yanatolewa, bahati mbaya hofu yangu imekua kweli.
Wamesimama watu wawili kuzungumza wa kwanza alipoanza kumtuhumi JPM juu ya kutoongeza mishahara ya watumishi TBC waka-mute sauti wakaweka watangazaji wa studio, amesimama Lema alipoanza tu kuzungumzia juu ya Tume ya Uchaguzi wame-mute tena wameweka watangazaji wa studio.
Sasa kwa mwendo huu atakaposimama TL mwenyewe si na matangazo mtazima?
Mlipoamua kurusha kampeni ya chama cha upinzani mlitarajia kuna mapambio ya sifa? Ili mradi hakuna matusi au maneno ya uongo acheni tusikie sisi wenyewe tutapima pumba na mchele.
TBC, TBC, TBC hamuwezi jua come November bosi wenu anaweza kuwa huyu huyu mnayetaka kumnyima fursa ya kusikika kwa ukamilifu.