Elections 2010 TBC1 na kindumbwendumbwe uchaguzi mkuu

awesome

Member
Joined
Oct 11, 2010
Posts
35
Reaction score
0
Zamani kiliitwa kipindi cha ''usiku wa habari'' kilichoanzishwa na bwn Muro kabla hajasimamishwa kwa tuhuma za kuomba rushwa kama ilivyoripotiwa na vyombo mblmbl ikiwemo TBC. Sasa kipindi kinajulikana kama ilivyoandikwa hapo juu.

Lakini sijaelewa muktadha mzima wa kipindi hiki bali kuonyesha au kunadi sera za ccm na kuonyesha kiduchu matukio ya vya pinzani. Huu ni utumiaje mbovu wa rasilimali za umma.
Kama tbc, chombo cha umma kinatumika kunadi chama tawala na kuacha vyama pinzani nyuma... hii ni ishara tosha ya kudidimiza democrasia nchini.

Hivi tbc hawana vipindi vya kurusha hewani?, kweli tbc inakera kuitazama, kwanza taarifa ya habari shallow inatangaza habari za dar na ccm tu. Bora ifungwe majengo tufugie bata.
 
Hawa jamaa wana udhaifu mwingi badala ya kurekebisha maproblem ya king'amuzi chao kibovu wanashobokea CCM na upupu wake. Huwa wanaboa sana..
 
..... NkURUGENZI NAYE KACHAKACHULIWA KITAMBO....
 
walishasema kuwa tv na redio haviwafikii wapiga kura wengi, je kwa nini wao wanabania wapinzania kutumia hizo stesheni?

kwa nini wao wanalipa mahela mengi kuhonga hizo stesheni ziwapendelee kwenye matangazo?
ipo namna
 
Hapa Tanzania,mfumo wa vyama vingi hupo kwa nadharia zaidi na si kwa vitendo.Wapinzania hawapewi fursa sana na chama tawala hii inatia kichefuchefu!
 
Historia haifutika na itakuja kuwahukumu...nazidi kushangaa kila siku, kulikoni watu wanashindwa kusoma alama za nyakati? Mie nawapa changamoto, wajiangalia miaka 10 ijayo na sio 1st november 2010.
 
Hivi tbc hawana vipindi vya kurusha hewani?, kweli tbc inakera kuitazama, kwanza taarifa ya habari shallow inatangaza habari za dar na ccm tu. Bora ifungwe majengo tufugie BATA

Nahisi ni sawa kabisaaaa ni bora tufugie bata mizinga na kuku wa nyama ili JWTZ wafanyie mazoezi na polisi kuwaogesha na maji ya UPUPU
 
walishasema kuwa tv na redio haviwafikii wapiga kura wengi, je kwa nini wao wanabania wapinzania kutumia hizo stesheni?

kwa nini wao wanalipa mahela mengi kuhonga hizo stesheni ziwapendelee kwenye matangazo?
ipo namna
Nyie andikeni habari zenu na mkiweza pelekeni kwenye redio na Tv zenu, bahati nzuri vijijini kwenyewe hawana umeme! - Makamba
 
Mi nadhani liundwe shirika lingine la utangazaji badala ya hili la TBC, DR Slaa baada tu ya kuingia magogoni kituo vituo vyote vya TBC vifungwe, hakuna kutoa kitu pale, kila mtu aende kulima wala hakuna haja ya kuwaruhusu kufanya kazi za utangazaji maana hawajui maadili ya kazi zao.
 
Nyie andikeni habari zenu na mkiweza pelekeni kwenye redio na Tv zenu, bahati nzuri vijijini kwenyewe hawana umeme! - Makamba

Ndugu yangu inaumiza sana hii kauli we acha tu, ina maana ni makusudi kwanini anasema bahati nzuri?
 
Tulioipigia kelele kauli hii tulionekana ni anti-CCM. Ikabidi tukae kimya, huenda wakubwa hawa hawakosei...! Au alikuwa anatania?
 
Back
Top Bottom