Nchi ya wavivu hii, yaani baadhi ya watu wanataka wakae pembeni ya runinga siku nzima wanafuatilia majibizano kati ya mawaziri wa CCM na wabunge wa upinzani badala ya kufikiria ni namna gani wataweza kuboresha hali zao za maisha. Nchi hii imejaa majungu, imejaa kila aina ya tabia inayofuga ujinga. Badala ya kufikiria kuzalisha ili pato la mtu mmoja mmoja na taifa liweze kuongezeka, wavivu wa kufikiri wanataka wapoteze muda wao wanafuatilia mijadala ya kina Lissu, Zitto na Nape!.
Mataifa makini yaliyopiga hatua, huweka utaratibu wa watoto zao kukaa mbali na TV mpaka wakati maalum, na ndio maana wanazalisha ziada ambayo inakuja kwetu katika mfumo wa misaada. Sisi tunaoishi kwa kuitegemea hiyo misaada, wala hatuoni aibu kufuga tabia za uvivu. Watanzania tunapotea, lazima turudi kwenye nidhamu ya maisha kama kweli tunataka kuwa Taifa litakaloheshimiwa kote duniani