TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Naomba kuuliza wadau,hivi zile nafasi 10 ambazo Rais ana mamlaka kisheria kuteua Wabunge ameshajaza zote?na kama bado n ngapi?
 
Nchi ya wavivu hii, yaani baadhi ya watu wanataka wakae pembeni ya runinga siku nzima wanafuatilia majibizano kati ya mawaziri wa CCM na wabunge wa upinzani badala ya kufikiria ni namna gani wataweza kuboresha hali zao za maisha. Nchi hii imejaa majungu, imejaa kila aina ya tabia inayofuga ujinga. Badala ya kufikiria kuzalisha ili pato la mtu mmoja mmoja na taifa liweze kuongezeka, wavivu wa kufikiri wanataka wapoteze muda wao wanafuatilia mijadala ya kina Lissu, Zitto na Nape!.

Mataifa makini yaliyopiga hatua, huweka utaratibu wa watoto zao kukaa mbali na TV mpaka wakati maalum, na ndio maana wanazalisha ziada ambayo inakuja kwetu katika mfumo wa misaada. Sisi tunaoishi kwa kuitegemea hiyo misaada, wala hatuoni aibu kufuga tabia za uvivu. Watanzania tunapotea, lazima turudi kwenye nidhamu ya maisha kama kweli tunataka kuwa Taifa litakaloheshimiwa kote duniani
 
Daaah nashukuru wazazi wangu kunipeleka shule niakelimika manyumbu wengi xana kama mtu anafurahia kuminywa kwa vyombo vya habari then
 
Idadi za wilaya zina umuhimu mkubwa sana kuliko kurushwa live kwa vipindi vya bunge, mleta mada usidanganywe na haya maisha ya kwenye majiji kama vile Dar, Arusha, Mbeya, Tanga na Mwanza. Maendeleo ni lazima yafike kila kona ya Tanzania, wananchi wanahitaji mifumo ya utawala kutokana na ongezeko la watu na ongezeko la mahitaji yao. Kumbuke kuwa asilimia chini ya 45 ya watanzania ndio wanaofikiwa na huduma ya umeme, hiyo 55 bado iko gizani. Wanaofuatilia vipindi vya bunge live wako ndani ya hiyo asilimia 45, hivyo kwao kufuatilia habari za bunge live hakuwezi kuwa ni muhimu kuliko uwepo wa wilaya mpya ambazo zinaundwa ili wananchi wengi waweze kufikiwa na huduma muhimu za kimaisha.
 
Umeongea Kama Nabii aliaye nyikani akiwaasa watu kutengeneza njia zao ili wafanikiwe.

Halafu wanaopigania kuonesha Bunge live Mikoa yao ni MARUFUKU kuwasha TV saa za kazi. Yaani Mikoa ya Kaskazini Kama umeolewa huko ukiwasha TV asubuhi wanakuwekea kikao cha ukoo. Wanaona kijana wao ameoa mke mufilisi na hivyo asipoangalia atakufa masikini!!!

Pia huku Kaskazini TV wanawawekea hao wazee kwaya na nyimbo mbalimbali na mahubiri ya dini. Sio kweli wakiwa hawana kazi wanaangalia Bunge. Ni urongo Wa mchana kweupe.

Ndio maana kaskazini hawataki watoto wao kuoa mabinti Wa Pwani. Issue hapa hawataki wanawake WAVIVU!!! Leo hii wanataka watoto Wa wenzao washinde kwenye TV?? Kweli akuuwae hakuchagulii silaha!!! Huu uchumi Wa kati tunaotaka kuuona hautapatikana kwa kuwashawishi watu wetu wawe WAVIVU!!!! Tena wakitoka kwenye TV Bunge likiisha wanaanza na mara wanataka mikutano, mara mtusindikize mahakamani, mara nk Sasa najiuliza watafanya kazi saa ngapi hawa vijana???

Vijana msiwe wajinga. Wenzenu watoto wao wako Ulaya wanapiga mzigo au elimu. Pia wana mabiashara ya kufa mtu. Nyie wanawatumia Kama big G ikiisha utamu wanatema. Amkeni cheapeni kazi acheni kulia lia kwamba ajira hakuna na huku hata kufanya kazi hamtaki.

TUNALAANI WALE WOTE WANAOSHAWISHI VIJANA WAPOTEZE MUDA KWENYE MATUKIO YASIO YA MAANA BADALA YA KUWAFUNDISHA KAZI AU BIASHARA ILI WAPATE KIPATO.

VIJANA SEMENI NOOOO!!! Kwenye hili kataeni kwa matendo na amkeni!!

Queen Esther

Tuendelee

Nchi ya wavivu hii, yaani baadhi ya watu wanataka wakae pembeni ya runinga siku nzima wanafuatilia majibizano kati ya mawaziri wa CCM na wabunge wa upinzani badala ya kufikiria ni namna gani wataweza kuboresha hali zao za maisha. Nchi hii imejaa majungu, imejaa kila aina ya tabia inayofuga ujinga. Badala ya kufikiria kuzalisha ili pato la mtu mmoja mmoja na taifa liweze kuongezeka, wavivu wa kufikiri wanataka wapoteze muda wao wanafuatilia mijadala ya kina Lissu, Zitto na Nape!.

Mataifa makini yaliyopiga hatua, huweka utaratibu wa watoto zao kukaa mbali na TV mpaka wakati maalum, na ndio maana wanazalisha ziada ambayo inakuja kwetu katika mfumo wa misaada. Sisi tunaoishi kwa kuitegemea hiyo misaada, wala hatuoni aibu kufuga tabia za uvivu. Watanzania tunapotea, lazima turudi kwenye nidhamu ya maisha kama kweli tunataka kuwa Taifa litakaloheshimiwa kote duniani
 
point of correction ni bil.4, MODs please badilisha heading.
 
Bosi hapo ni mil. 4 au bil.4??
Anyway, hio ndo serikali mlioichagua hata mkisema kua wananchi mtachangia ilimrad lioneshwe live bado watabisha na mtapewa sababu mpaka mtakaa...
 
Bosi hapo ni mil. 4 au bil.4??
Anyway, hio ndo serikali mlioichagua hata mkisema kua wananchi mtachangia ilimrad lioneshwe live bado watabisha na mtapewa sababu mpaka mtakaa...
Nimeliona kosa nimewaomba mods wanisaidie kubadilisha.
 
Wakikuambia wanabana matumizi za kuambiwa changanya na zako. Hii ndio Tanzania Na mkutano wao utakuwa live hii ndiyo Tanzania
 
Nadhani za chama ni za chama na za bunge ni za serikali. Au serikali hukipatia chama fedha kwenye shughuli za chama?
 
Back
Top Bottom