Tulishasema Tanzania hakina Demokrasia na kujishau tu hamkutuelewa. Sasa mnaona CCM inakotupeleka?
Watarudia kuonyesha kuanzia saa nne usiku baada ya kuhaririwa
Sasa hizo pesa za kulipia vipindi vya bunge nadhani ni sehemu ya kodi zetu swali langu ni kuwa je TBC hawapati ruzuku toka serilkalini au nayo imebinafsishwa kama UDA ,na kama wanapata sasa kigugumizi cha nini wakati wananchi ndio wanaiwezesha ? Kuna baadhi ya vipindi havina manufaa kwa jamii na wanavionyesha huwa vinagharamiwa na nani ,au ndo hawataki wananchi waone mawaziri mizigo wakichambuliwa ?Nape:
Anatangaza kuwa TBC
itakuwa inatangaza baadhi
ya matukio ya Bunge
Lengo ni kubana
matumizi..
Anasema gharama za kuendesha Bunge zimefikia 4Bln kwa Mwaka.
Anasema kutakuwa na
kipindi maalum kitakachokuwa kinarushwa usiku kuanzia saa 4 hadi 5 Usiku.
.
Statv nao wamekata gafla badala yake wameweka VOA. Nimeishiwa poz yaniHaina shida, ikiwezekana wazime kabisa matangazo yao, mbona tutaangalia kupitia STAR TV, live wao wanaonyesha
ha ha haaa
Unaonaje wakiwa wanazima mitambo yote ya simu pia ili uwe unafanya kazi
Fanya kazi wewe acha uvivu, nchi haijijengi!!
Unaonaje wakiwa wanazima mitambo yote ya simu pia ili uwe unafanya kazi
Zama za msoga mtazikumbuka sana maana aliachia watu mkosoe mnavyotaka sasa hapa kazi tuu
CCM wako predictable ile mbaya ..,. haya yote yalibashiriwa ... kama kweli serikali ya Magufuli iko kwaajili ya wananchi hofu ya nini?Katika kauli za Mawaziri, Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye, ametangaza kwamba, Kuanzia tarehe 26 Januari mwaka 2016, TBC1 haitaonesha tena Mikutano ya bunge live kutokana na gharama za kuonesha live kufikia bilioni nne kwa mwaka.
Badala yake TBC1 watarekodi na kuonesha katika kipindi maalum usiku kuanzia saa nne hadi saa tano.
Hii itanyima wanchi fursa ya kuona kinachoendelea Bungeni.
Kama tatizo ni gharama, basi wapunguze posho za wabunge, mawaziri na Makatibu, na mishahara yao pia japo kwa 5%. Itatosha na kubakiwa na kiasi kikubwa cha kuendelea kurusha live kwa miaka miwili mbele.
Hebu tingisha kichwa chako kidogo, je unahisi nini?Safi sana hiki kilikuwa ni kilio changu siku zote, Watu wafanye kazi na waache kuangalia Bunge, mkirudi nyumbani jioni baada yakazi mtaangalia Bunge tani yenu au kama mmechoka hata wkend!
Safi sana W. Nape!
NA Bado Tutasikia Mengi Mno!!! Tusubirie Tu!!! Tehe! Tehe! Tehe!!! KUNA Hidden Ajenda Tu, Huyo Aliyetangaza, Si Ndio Katibu Wa Itikadi Na Uenezi!!!!!??? Ngoja Tusubirie Tuone Na Tusikie!!!!Hii nayo kali aisee
Nmemsikiliza nkachoka
Tv ya Taifa inashindwa kurusha matangazo ya bunge kweli
Hapana aisee hii serikali yaanza nitia shaka