TBL: Kuleni chakula kabla ya kunywa

TBL: Kuleni chakula kabla ya kunywa

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Ili kufikia lengo la kupunguza matumizi ya pombe hatarishi kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2025, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imezindua kampeni ya Mdogomdogo inayohamasisha unywaji pombe usiozidi kipimo ambao ni hatari kwa afya ya watumiaji.

Uzinduzi wa kampeni hiyo umekwenda sambamba na uongezaji wa alama nyingine mbili ambazo zinahamasisha kula na kunywa maji mengi kabla ya kunywa na kunywa kistaarabu.

Alama hizo mbili zilizoongezwa kuungana na tatu zilizokuwapo awali zilizokuwa zikizuia matumizi ya pombe kwa walio na umri wa chini ya miaka 18, kuzuia matumizi ya pombe kwa wajawazito na kutoendesha gari baada ya kunywa.

Hayo yameelezwa katika uzinduzi wa kampeni hiyo inayotarajiwa kudumu kwa miezi 9 hadi Desemba mwaka huu.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo jana Machi 22, Mesiya Mwangoka ambaye ni Mkurugenzi wa Masuala ya Mahusiano na maendeleo uendelevu wa TBL amesema alama inayohamasisha kula kabla ya kunywa imeongezwa.

Amesema uongezwaji huo umefanyika baada ya utafiti kubaini kuwa kula na kunywa maji mengi kunapunguza uwezo wa mtu kunywa pombe nyingi.

“Unapokula chakula kiwango cha unywaji bia kinashuka, ile bia inaenda taratibu kwa sababu tumbo limejaa tayari na kuna tofauti kubwa ya unywaji imeonekana kati ya yule aliyekula na kushiba na yule anayekunywa bila kula,” amesema Mesiya.

Amesema mtu anapokuwa amekula haimsadii tu kupunguza kiasi cha pombe anachokunywa bali pia kuwa na nguvu na kuzuia mwili wake kudhoofika.

Kampeni ya mdogomdogo pia imelenga kukuza utumiaji bora wa pombe usioathiri desturi za kijamii na tabia ya mtu binafsi na kupunguza matumizi hatari ya pombe.

John Blood ambaye ni Mkuu wa masuala ya kisheria ya kampuni, ABInBev amesema ni muhimu kusaidia watumiaji kuelewa jinsi pombe inapaswa kutumiwa kwa kuzingatia ukomo.

“TBL inahakikisha kuwa masoko yao hayalengi watumiaji wa chini ya umri wa miaka 18, kampuni inalenga kuepuka kukuza utumiaji wa pombe hatarishi au tabia hatarishi zinazotokana na pombe,”

MWANANCHI
 
Kwa maoni yangu ukila na kushiba vizuri maana yake ni kwamba utakuwa na uwezo mkubwa wa kunywa bia nyingi zaidi kuliko anayekunywa bila kula. Aisee huyu aliyebuni hii kampeni ni very genius baada ya kuona mauzo yanashuka kwa bei ya kongoro, mkia, nyama choma, mishikaki kupanda hahaaaaa....
 
Wanapunguza unywaji kwa kuongeza stika duh [emoji1]
Kama kweli wanataka kupunguza unywaji wa pombe wapunguze uzalishaji
Hamna wajanja hawa... Ukiwa umeshiba unachelewa kulewa kuliko ukiwa na njaa

Usipokula tuseme utalewa bia ya nane hvi

Sasa ukianza na kutimoto nusu na robo na maji lita moja unaeza kunywa bia 20..

Yan wanaongeza mauzo hapo[emoji1787][emoji1787]
 
Kabisa ukishiba ongeza na kunywa maji mengi hauwezi kulewa kirahisi
 
Ili kufikia lengo la kupunguza matumizi ya pombe hatarishi kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2025, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imezindua kampeni ya Mdogomdogo inayohamasisha unywaji pombe usiozidi kipimo ambao ni hatari kwa afya ya watumiaji.

Uzinduzi wa kampeni hiyo umekwenda sambamba na uongezaji wa alama nyingine mbili ambazo zinahamasisha kula na kunywa maji mengi kabla ya kunywa na kunywa kistaarabu.

Alama hizo mbili zilizoongezwa kuungana na tatu zilizokuwapo awali zilizokuwa zikizuia matumizi ya pombe kwa walio na umri wa chini ya miaka 18, kuzuia matumizi ya pombe kwa wajawazito na kutoendesha gari baada ya kunywa.

Hayo yameelezwa katika uzinduzi wa kampeni hiyo inayotarajiwa kudumu kwa miezi 9 hadi Desemba mwaka huu.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo jana Machi 22, Mesiya Mwangoka ambaye ni Mkurugenzi wa Masuala ya Mahusiano na maendeleo uendelevu wa TBL amesema alama inayohamasisha kula kabla ya kunywa imeongezwa.

Amesema uongezwaji huo umefanyika baada ya utafiti kubaini kuwa kula na kunywa maji mengi kunapunguza uwezo wa mtu kunywa pombe nyingi.

“Unapokula chakula kiwango cha unywaji bia kinashuka, ile bia inaenda taratibu kwa sababu tumbo limejaa tayari na kuna tofauti kubwa ya unywaji imeonekana kati ya yule aliyekula na kushiba na yule anayekunywa bila kula,” amesema Mesiya.

Amesema mtu anapokuwa amekula haimsadii tu kupunguza kiasi cha pombe anachokunywa bali pia kuwa na nguvu na kuzuia mwili wake kudhoofika.

Kampeni ya mdogomdogo pia imelenga kukuza utumiaji bora wa pombe usioathiri desturi za kijamii na tabia ya mtu binafsi na kupunguza matumizi hatari ya pombe.

John Blood ambaye ni Mkuu wa masuala ya kisheria ya kampuni, ABInBev amesema ni muhimu kusaidia watumiaji kuelewa jinsi pombe inapaswa kutumiwa kwa kuzingatia ukomo.

“TBL inahakikisha kuwa masoko yao hayalengi watumiaji wa chini ya umri wa miaka 18, kampuni inalenga kuepuka kukuza utumiaji wa pombe hatarishi au tabia hatarishi zinazotokana na pombe,”

MWANANCHI
Wale wanywa shimha ndo wanatabia za kunywa bila kula. Alf wakitoka hapo wanatembea juani baad ya muda wanaanza kutoka moshi mwilini
 
Shida yote hii ya nini? Kama ina madhara ni rahisi tu. Stop production!

Sasa wanawatengenezea halafu wanafanyia kampeni ya kupunguza kunywa ya niji sasa?
 
Back
Top Bottom