TBL na Serengeti Bia

TBL na Serengeti Bia

Ushindani wa namna hii kati ya TBL na SBL ni wa kipuuzi mno? Tangaza ubora wa bidhaa zako, and thats enough!Nadhani PEPSI na COCACOLA nao wana kamtindo kakishenzi namna hii.

Umefuliaaaaaaaaa....! Serengeti ipo juu sana tu..!
 
Wakuu kitu ya SERENGETI iko pahala pake
Kitu muhimu TBL wanatakiwa kufanya ni kubadili department nzima ya R&D nadhani hawajui watendalo kwenye soko hili la ushindani
 
Hatimaye TBC wamerusha live jana ule ufisadi unaofanywa na TBL kwa kabia ketu ka Serengeti. SBL wanadai wana vielelezo vya kutosha na wameandika barua FCC. Kazi hipo kwa hawa walipa kodi wakubwa kama anavyodai Bado nipo nipo!
 
Binamu Chrispin um eisikia hiyo ya SBL kufile complain yao FCC, huenda sasa chui akarejea alikokuwa kafungiwa. Chui anaadhibiwa kama viongozi wa soka wa majimaji/songea walivyofanyiwa na TFF?
 
Binamu Chrispin um eisikia hiyo ya SBL kufile complain yao FCC, huenda sasa chui akarejea alikokuwa kafungiwa. Chui anaadhibiwa kama viongozi wa soka wa majimaji/songea walivyofanyiwa na TFF?

Mpwa mi hata sikuona upungufu wake. Nilishatahadharisha, hata wamfanyeje ikibidi ntamfuata hukohuko Mbugani Serengeti.
 
Kwa mujibu wa magazeti ya Kiswahili ya leo, vita ya hawa mafahali wawili wa bia imeshafika mezani kwa Pinda.
Let's hope for the worst.
 
TBL wanatufanya watanzania midoli! Wametoa tangazo lao kwenye gazeti la Mwananchi kuiponda SBL halafu wanadai ni wananchi!
 
TBL awmefuli hata wafanye nini hawapati kitu na kile kiwanda wanachofungua kule mbeya labda wawa uzie wamalawi na wasumbiji Tz hampati kitu na Ma fire extinguisher yenu
 
Mgogoro wa TBL, SBL watinga bungeni
Thursday, 29 October 2009 16:42
Na John Daniel, Dodoma

MBUNGE wa Busega, Bw. Raphael Chegeni (CCM), amemtaka Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kueleza kama anatambua mvutano wa kibiashara uliopo kati ya kampuni mbili za bia, Serengeti Breweries (SBL) na Tanzania Breweries (TBL) unaotishia amani ya nchi.

Akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni jana, Bw. Pinda alikiri kuwepo kwa mvutano huo na kwamba tayari amekutana na baadhi ya wahusika akiwemo Jaji Mark Bomani (Mwenyekiti wa Bodi ya Serengeti) na kuzungumzia tatizo hilo.

Katika swali lake la nyongeza Bw, Chegeni, alimtaka Bw. Pinda kuona umuhimu wa kushughulikia suala hilo kwa karibu na hatua zaidi kuchukuliwa haraka kwa kuwa moja ya washindani hao ameagiza kung'olewa kwa mabango ya mshindani mwezake kwa kuyapiga mawe, jambo ambalo ni kinyume na ushindani wa kibiashara na hatari kwa amani
na utulivu wa nchi.

Bw. Pinda alisema serikali haiwezi kuingilia kati tatizo hilo moja kwa moja kwa kuwa ipo mamlaka iliyoundwa kisheria kwa lengo la kushughulikia ushindani wa haki katika biashara bali serikali inaweza kuingilia kati pale tu inapojiridhisha kwamba tume hiyo ya ushindani imeshindwa kumaliza tatizo hilo.

Mgogoro huo umekuwa wa muda mrefu na hivi karibuni iliripotiwa kuwa kampuni mojawapo imewahonga baadhi ya wamiliki wa baa ili wasiuze bia za washindani wao.

Source: Gazeti la Majira

My Take:

TBL wamechemka vibaya mno katika mbinu yao hii chafu ya kupambana na ushindani unaotolewa na SBL.Tutegemee haki itatendeka katika kulishughulikia suala hili.FCC waachwe wafanye kazi yao kwa uhuru maana inavyoelekea SIASA inaanza kuchukua mkondo wake kwenye hili(wanasiasa washavamia tayari).Tutegemee maamuzi ya HAKI kutoka FCC na si vinginevyo...TBL wamefulia mbaya zama hizi(kwa mtizamo wangu)
 
Nyingine hii kutoka Gazeti la Habari Leo

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, ameagiza kuwa, kama kuna kampuni inayotengeneza bia inaona wapinzani wake kibiashara wanaionea iwasilishe malalamiko kwenye tume ya ushindani wa biashara(FCC).

Pinda amewataka wawekezaji wa kigeni na wa ndani waelewe na kukubali kwamba, mfumo wa kibiashara unaotumika nchini ni wa ushindani katika soko huru.

Ameyasema hayo bungeni leo wakati anajibu swali la papo hapo aliloulizwa na Mbunge wa Busega, Dk Raphael Chengeni.

Waziri Mkuu amesema, licha ya kutoelewa kwa undani vita inayoendelea kati ya Kampuni ya Bia (TBL) na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SLB), za Dar es Salaam,wawekezaji hao wanapaswa kukitumia chombo kilichoundwa kisheria kusimamia ushindani wa kibiashara.

"Kama kuna kampuni inaona inaonewa bila sababu wachukue hatua ya haraka kukitumia chombo hicho kama ataona ana sababu ya msingi ya kufanya hivyo."

Dk Chegeni alitaka kufahamu Serikali inachukua hatua gani kuhusu vita kati ya kampuni hizo hasa ile ya kuvunjiana mabango kwa madai kuwa inaweza kuhatarisha amani.

Pinda amelieleza Bunge mjini Dodoma kuwa, amefanya vikao na Mwenyekiti wa kampuni ya Serengeti, Jaji Mark Bomani, na kumshauri kuwa si busara kuiuza kwa wageni kampuni iliyoanzishwa na wazalendo.
 
Mgogoro wa TBL, SBL watinga bungeni
Thursday, 29 October 2009 16:42
Na John Daniel, Dodoma

MBUNGE wa Busega, Bw. Raphael Chegeni (CCM), amemtaka Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kueleza kama anatambua mvutano wa kibiashara uliopo kati ya kampuni mbili za bia, Serengeti Breweries (SBL) na Tanzania Breweries (TBL) unaotishia amani ya nchi.

Akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni jana, Bw. Pinda alikiri kuwepo kwa mvutano huo na kwamba tayari amekutana na baadhi ya wahusika akiwemo Jaji Mark Bomani (Mwenyekiti wa Bodi ya Serengeti) na kuzungumzia tatizo hilo.

Katika swali lake la nyongeza Bw, Chegeni, alimtaka Bw. Pinda kuona umuhimu wa kushughulikia suala hilo kwa karibu na hatua zaidi kuchukuliwa haraka kwa kuwa moja ya washindani hao ameagiza kung’olewa kwa mabango ya mshindani mwezake kwa kuyapiga mawe, jambo ambalo ni kinyume na ushindani wa kibiashara na hatari kwa amani
na utulivu wa nchi.

Bw. Pinda alisema serikali haiwezi kuingilia kati tatizo hilo moja kwa moja kwa kuwa ipo mamlaka iliyoundwa kisheria kwa lengo la kushughulikia ushindani wa haki katika biashara bali serikali inaweza kuingilia kati pale tu inapojiridhisha kwamba tume hiyo ya ushindani imeshindwa kumaliza tatizo hilo.

Mgogoro huo umekuwa wa muda mrefu na hivi karibuni iliripotiwa kuwa kampuni mojawapo imewahonga baadhi ya wamiliki wa baa ili wasiuze bia za washindani wao.

Source: Gazeti la Majira

My Take:

TBL wamechemka vibaya mno katika mbinu yao hii chafu ya kupambana na ushindani unaotolewa na SBL.Tutegemee haki itatendeka katika kulishughulikia suala hili.FCC waachwe wafanye kazi yao kwa uhuru maana inavyoelekea SIASA inaanza kuchukua mkondo wake kwenye hili(wanasiasa washavamia tayari).Tutegemee maamuzi ya HAKI kutoka FCC na si vinginevyo...TBL wamefulia mbaya zama hizi(kwa mtizamo wangu)

Bila shaka na wewe umathirika sana na hii huduma ya serengeti mkuu Balantanda!

Umeona mwananchi ya leo wanavyojaribu kutu-fool hawa TBL, ama kweli wameishiwa. Kizuri chajiuza bwana, wanalalamika eti Serengeti haipaki rangi kwenye mabaa kama ofa kwa wamiliki na kutoa mafunzo kwa wahudumu ndio maana haiuzwi, WHAT A SHIT! Pumba tupu, CHUI anachanja mbuga haitaji promo Za majitaka!
 
Ukisoma kwa uangalifu lile tangazo la gazeti la Mwanachi leo utaona kuwa ni inside plot ya kampuni moja ya bia dhidi ya nyingine. Wafanyabiashara wa mabaa Dar hawana umoja wao, hawana viongozi, hawajawahi kufanya mkutano hata siku moja kuzungumzia hali hii. Sana sana huwa wanakaribishwa na makampuni hayo kwenye tafrija mbalimbali zinzotayarishwa na makampuni hayo. Walikaa lini wakakubaliana kuandika yaliyoandikwa kwenye tangazo hilo?
Kama wangekuwa na umoja na wakafanya mkutano na kutoa azimio la kuandika tangazo kama linavyoonekana kenye gazeti la Mwananchi leo ingekuwa habari, isingekuwepo haja ya kutoa tangazo.
Alichokifanya mwandishi wa tangazo hili ni kutumia Kiswahili kibovu kisicho na mpangilio imara ili ionekane kuwa limeandikwa na wafanyabiashara wasio na elimu ya kutosha.
 
Back
Top Bottom