TBS yateketeza Vipodozi vyenye viambato sumu na bidhaa zingine zilizokwisha Muda wa matumizi zenye thamani ya takribani Sh. Milioni 400

TBS yateketeza Vipodozi vyenye viambato sumu na bidhaa zingine zilizokwisha Muda wa matumizi zenye thamani ya takribani Sh. Milioni 400

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) yateketeza bidhaa zenye thamani ya takribani Sh Milioni 400 bidhaa hizo hazikidhi Viwango vya ubora na kuisha Muda wake wa matumizi. Kwa upande wa Vipodozi ni vile vyenye viambato sumu zisizofaa kwa matumizi kwa binadamu.

Dk. Kandida P. Shirima (Kaimu Mkurugenzi, Usimamizi na utekelezaji wa Sheria TBS amesema Lengo la TBS kuteketeza bidhaa hizo ni kulinda Afya za watumiaji.

Dk. Kandida amesema bidhaa na Vipodozi hizo zimekamatwa katika Mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro ikiwa sehemu ya utekelezaji wa Majukumu ya TBS kufanya Ukaguzi wa mara kwa mara .

Hata hivyo bidhaa tunazoteketeza hapa leo katika Tanuru letu la Mkuranga Zina takribani uzito wa tani 9 na zinathamani takribani Sh. Milioni 400.

"Pia niwatake Wananchi kutotumia bidhaa zilizokwisha Muda wake pamoja na kutotumia Vipodozi vyenye viambato Sumu maana ni hatari kwa Afya ya mtumiaji" - Dk. Kandida Shirima.

"Niwaombe wananchi kukagua bidhaa kabla ya kutumia ili kujua Muda wa matumizi pamoja na viambato vilivyotumika kutengeneza bidhaa hizo ili kuwa salama zaidi kwa mtumiaji" - Dk. Kandida Shirima
 

Attachments

  • 20220831_080649.jpg
    20220831_080649.jpg
    67.9 KB · Views: 8
  • 20220831_080653.jpg
    20220831_080653.jpg
    49.5 KB · Views: 8
  • 20220831_080656.jpg
    20220831_080656.jpg
    104.5 KB · Views: 8
  • 20220831_080700.jpg
    20220831_080700.jpg
    65.8 KB · Views: 8
Taniru la kuteketeza hizo bidhaa feki au zilizoisha muda wake wa matumizi linafanyaje kazi ?. Kama mnateketeza kwa moto, hamuoni kuwa moshi unaotokana na kuteketeza vipodozi unapanda juu na kuchafua mazingira zaidi na baadaye kuwadhuru wananchi ?, Vipi huo uchafuzi wa hewa utakapokuja kutengeneza mvua ya tindikali? .... Mtalaumu tabianchi ?
 
Back
Top Bottom