TBS yatoa ufafanuzi kuhusu viuatilifu vinavyotumika katika kilimo cha mbogamboga

TBS yatoa ufafanuzi kuhusu viuatilifu vinavyotumika katika kilimo cha mbogamboga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na majukumu mengine hufanya ufuatiliaji wa bidhaa za mbogamboga ili kuhakiki usalama wake. Kilimo cha mazao ya mbogamboga, hutumia viuatilifu ili kukabiliana na wadudu waharibifu, magonjwa ya mimea na magugu ambapo viuatilifu vinavyotakiwa kutumika ni vile vilivyoidhinishwa na mamlaka za udhibiti.

Pia soma ~ Ukweli Usiosemwa: 'Mboga zenye Viwatilifu vyenye viambata vya sumu' zinavyohatarisha afya za maelfu ya wananchi wa mijini

Ufuatiliaji na uchunguzi wa kimaabara wa aina mbalimbali za mbogamboga katika soko umeonesha kuwa mazao hayo hayana mabaki ya viuatilifu (pesticide residues) yanayozidi kiasi kinachovumilika (maximum residue limit) kwa mujibu wa viwango vya WHO/FAO.

TBS itaendelea kufanya ufuatiliaji wa bidhaa za mbogamboga na kushirikiana na Mamlaka inayohusika na udhibiti wa afya ya mimea na viuatilifu ili kuhakikisha usalama wa mbogamboga unazingatiwa na wadau wote katika mnyororo wa thamani.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja kwa namba 0800110827.

Imetolewa na:
JAMHURI
TANZANIA
Gladness H. Kaseka WA Maneja wa Uhusiano na Masoko


TBS.jpg
 
Utafikiri yako siriazi. Wakati tumegeuka dampo la bidhaa feki. Imagine 86% ya pombe zote hapa Bongo ni feki. Na yapo tu yanavuta vitambi kwenye viyoyozi pale Ubungo 🚮🚮🚮🚮🚮
 
Back
Top Bottom