TBT: Ajali ya moto Morogoro (2019), ni lipi la kujifunza?

TBT: Ajali ya moto Morogoro (2019), ni lipi la kujifunza?

2019,Monday, August 12,Idd El Adha.
So, tell me what you think.

Siku Ile Waislamu walikuwa wana sherehe.
Nikaenda kwenye kijiwe nikauliza ", Waislamu wanasherehekea nini leo?"
Nikaambiwa,"Idd El Adha,,"
Nikasema,"Oh, what's that?"
Nikaambiwa siku Abraham alipoamriwa kumtoa sadaka mtoto wake.
Basi nikajibu,in my usual careless way,
"Oh,now it is clear to me,Ile ajali mbaya imetokea Morogoro jana,na sasa Waislamu wanasherehekea Idd El Adha. Oh,I understand everything.."
 
Naomba nisiadithie lakini kwa ufupi sana ni kwamba nilipoteza watu wangu wawili wa karibu nikiwaona wanateketea huku sijui nini chakufanya
Mbona nilisikia wengi wao walikuwa mateja pale
 
Hee sijaziona hizi aisee
Ndani ya mwezi huu october 2024 nigeria na uganda wamepotea watu karibia 200 kwa kuchota mafuta.

Umaskini wetu unasababisha watu kutowaza athari zinazoweza kutokea bali kufikiri tu fursa iliyopo mbele yake.
 
Nimejifunza kitu kimoja pesa ya haraka haraka ipo Ila "Kuna aslimia kubwa za kuupoteza uhai mapema" kwa kusaka pesa za haraka maana hapa watu walijua wakiuza mafuta ni pesa ya fasta fasta
2.kuendelea kuomba mwisho mwema
Kwenye tarehe 10 Agosti 2019, Tanzania ilikumbwa na tukio la kusikitisha na kutisha ambalo limebaki kuwa kumbukumbu mbaya kwa wengi.

Ajali ya moto iliyotokea mjini Morogoro, karibu na eneo la Msamvu, ilihusisha lori la mafuta lililopinduka na kulipuka, na kupelekea vifo vya watu zaidi ya 100. Tukio hili lilitokeza huzuni na mshtuko kwa taifa na kuacha alama isiyofutika kwenye historia ya nchi.
Tukio lilianza pale ambapo lori la mafuta lilipata ajali na kupinduka. Baada ya kuanguka, watu wengi walikusanyika kwa haraka kuchota mafuta yaliyokuwa yakimwagika kwenye eneo la tukio. Watu walijitokeza kutoka maeneo mbalimbali wakiwa na ndoo, madumu, na chupa ili kupata mafuta. Baadaye, ghafla moto ulilipuka kwenye eneo hilo, na kusababisha maafa makubwa kwa waliokuwa karibu.


Pamoja na kwamba haijathibitishwa chanzo rasmi cha moto, baadhi ya mashuhuda walieleza kuwa ulitokana na cheche za moto kutoka pikipiki au sigara iliyokuwa ikivutwa karibu na eneo la tukio. Mlipuko huo ulitokea ghafla na kuteketeza eneo zima, ukiwaacha watu wakiwa wamejeruhiwa vibaya na kuharibu mali zao.


Mara baada ya tukio hilo, viongozi wa kitaifa walitembelea eneo la ajali ili kutoa pole kwa waathirika na kushuhudia hali ya kusikitisha iliyotokea. Rais wa wakati huo, John Pombe Magufuli, alitangaza siku ya maombolezo ya kitaifa kwa heshima ya waliopoteza maisha. Viongozi wa kidini na wa kijamii pia walitoa misaada na ushauri kwa familia za waathirika na walitoa wito kwa Watanzania kuwa makini na ajali kama hizi.


Ikiwa leo ni alhamisi ya TBT, tukio la moto la Morogoro limebaki kuwa la kihistoria kwa taifa. Kwa pamoja, tunapaswa kujifunza kutokana na ajali kama hizi, kuwa makini na tahadhari, na kuhamasisha jamii kuhusu hatari zinazoweza kutokea. Em tuambie, Ulipata Funzo gani kutokana na Ajali hii?


Mwisho, napenda kutoa pole kwa familia zote ambazo zilipoteza wapendwa wao kwenye ajali hii na tunaiomba serikali iendelee kuchukua hatua kuhakikisha usalama wa raia wakati wa dharura kama hizi.​
 
Unatonyesha vidonda yani ili tukio nimelishuhudia kwa macho yangu bila kuadithiwa kwakweli huwa sitamani kulikumbuka kabisa
Pole sana mkuu, ni tukio liliotowesha watu wengi uhai na mali. Lkn ni kama halijawahi kutokea nchini. Sijui watu wa fire wanakosaje ubunifu wa kuwa na elimu na kufanya kumbukumbu za matukio mabaya kama haya.
 
Kuna waziri aliulizwa "...umejifunza nini kutokana na hili, akajibu nimejifunza MOTO NI KIBOKO"
 
Back
Top Bottom