TBT: "Bongo Dar es Salaam" hii ngoma Prof Jay alikuwa mbele ya wakati sana. Respect legend

Ila jaman mbona mnatuonea Kila kitu hatuwez elewa khee💔
Nakuwekea Audio/ Video: Bongo Dar Es Salaam (feat. Lady Jaydee)
Your browser is not able to display this video.

VERSE 1:
Yoh, yoh, yoh
Ndani ya Bongo mambo super hapana ubongo
Ingawa sometime Bongo chungu kama sifongo
Nafanya makaratee kama machinga mtaa wa Congo
Kimtindo mtindo nakata ngebe vimtima nyongo
Your browser is not able to play this audio.
 
Alianza

Prof Jay ft Jide - Bongo Dar es Salaam

Jay Z ft Alicia Keys - Empire state of mind (New York)

Prof Jay ft Simple X & Sos B - Piga Makofi

Busta Rhymes - Make it clap

Sasa hivi naona yuko poa
​
Unataka kusema amekopi na kupesti mkuu,,kama ndivyo basi ni idea nzuri,si vibaya kufanya hivyo,hata china imepiga hatua kwa kupata ideas kutoka kwa waliokuwa wamewatangulia kimaendeleo,hadi sasa wamekuwa tishio kwao.
 
"Hizi zinapoyeyuka wabongo tunalia ukata"
hapo kwenye bold ni deals.


dumba kali saa moja shuka utosini.
dumba ni jua.

Wanatamani wangezaliwa Blue nay wamwage radhi
Blue nay ni brunei

Bonge moja na ngoma ila kwangu mimi naikubali sana ngoma ya Chemsha Bongo
 
Ok asante kwa kuweka sawa mimi nilicopy tu lyrics kutoka mtandaoni

Waandika lyrcis wa nyimbo za bongo flava huwa wanakosea sana sijui ni kwa nini?
​
 
Ok asante kwa kuweka sawa mimi nilicopy tu lyrics kutoka mtandaoni

Waandika lyrcis wa nyimbo za bongo flava huwa wanakosea sana sijui ni kwa nini?
​

Yap lyrics za mitandoani zina small mistakes .
Hizi nyimbo ndizo ziianza kufanya madingi zetu waanze kuona nyimbo za bongo fleva zina jumbe zamaana na sio uhuni
Nakumbuka sikuhizo nasikiliza ngoma ya chemsha bongo home ilipoisha msure aliniambia embu irudie hiyo nyimbo .
 
Ndugu mwandishi nyingine ni mtazamo ambayo yupo na sola thang pamoja mgambo sele
 
Beat yake tunaimba🔜🔙🔛🔝🔚
 
Hizi nyimbo ndizo ziianza kufanya madingi zetu waanze kuona nyimbo za bongo fleva zina jumbe zamaana na sio uhuni
Nakumbuka sikuhizo nasikiliza ngoma ya chemsha bongo home ilipoisha msure aliniambia embu irudie hiyo nyimbo
Umesema vyema

Hata baadhi ya washua walianza kuikubali bongo flava waliposikia ngoma yake ya "Chemsha bongo"

Jay kafanya mapinduzi makubwa sana kwenye Bongo Flava na hip hop mpaka ikubalike katika jamii

Unajua Jay kwenye ngoma ya "Utaniambia nini" kuna sehemu anasema

​
Ah kwenye mziki nilianza kabla yako
Shahidi mama yako utaniambia nini?

Mijengoni nilikuwa na baba zako
Wengine mama zako, utaniambia nini?

​
Alikuwa sahihi sana kuimba hivyo leo kuna madogo na wasanii wakubwa tu wenye majina katika kiwanda cha muziki wa Bongo ila wazazi wao ni mashabiki wakubwa wa Prof.

Wampe heshima yake huyu mkongwe
​
 
Ndugu mwandishi nyingine ni mtazamo ambayo yupo na sola thang pamoja mgambo sele
Chifu hiyo ni ngoma bora ya wakati wote ya collabo katika Bongo hip hop. Humo vichwa vilitulizwa vikaandika mashairi ya kina sana

Kuna hii punch line ya Jay huwa lazima ije akilini kila mara nikisia mtu anautaja huo wimbo

​
Wanakwenda hatua mbili, wanarudi kumi na kujipongeza,
Bila kuzingatia hatua nane walizopotеza,
Hao ni mafukara wa akili zao’ na uwezo wao
​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…