Mzee wa kupambania
JF-Expert Member
- Aug 14, 2022
- 21,767
- 54,912
Siki hizi wasanii wa rap hawana ubavu wa kuandika verse 3 zilizoshiba kama alizokuwa anafanya prof jay wimbo huo wa Bongo DSM una dk 5:37 na hauchoki kuusikiliza
Zote za prof jizz ni kali sana ref zile series ya ndiyo mzeeChifu hiyo ni ngoma bora ya wakati wote ya collabo katika Bongo hip hop. Humo vichwa vilitulizwa vikaandika mashairi ya kina sana
Kuna hii punch line ya Jay huwa lazima ije akilini kila mara nikisia mtu anautaja huo wimbo
Wanakwenda hatua mbili, wanarudi kumi na kujipongeza,
Bila kuzingatia hatua nane walizopotеza,
Hao ni mafukara wa akili zao’ na uwezo wao
Siku izu utaskia nakuwa haraka kama nakula mbolea mara mwingine utaskia shipupy shipupySiki hizi wasanii wa rap hawana ubavu wa kuandika verse 3 zilizoshiba kama alizokuwa anafanya prof jay wimbo huo wa Bongo DSM una dk 5:37 na hauchoki kuusikiliza
Albamu ya Machozi,Jasho na Damu ndio Albamu yangu bora toka Muziki wa Bongo Flava uanze Tanzania
Jamaa walilazimika kutumia akili kubwa sana kuja na ngoma kali sana zinazoishi muda mrefu ili kujijenga kijamii.
Saivi bongo flava ni singeli ni maajabu ya duniaVERSE 1:
Yoh, yoh, yoh
Ndani ya Bongo mambo super hapana ubongo
Ingawa sometime Bongo chungu kama sifongo
Nafanya makaratee kama machinga mtaa wa Congo
Kimtindo mtindo nakata ngebe vimtima nyongo
Hapana matata kitu roho inapenda mtapata
Bongo Dar Es Salaama ni mpeto wa kutakata
Nenda viwanja vikali vya Bongo ustaajabu
Na pita Sleepway, Blue Pam au Mambo Club
Kama hujazoea unaweza ukavunja shingo
Mambo Isidingo watu mkononi Nokia bingo
Huwezi kujua yupi mtoto wa geti, yupi changu
Wote wanameremeta kama mamtoni mwanangu
Hizi zinapoyeyuka wabongo tunalia ukata
Subiri kichapo chake pale mbongo anapozipata
Mwendo wa kiti kirefu jirani na nyama choma
Na toto mbili tatu za geti au za kona
Hii watu wa Bongo tunasema napoteza mawazo
Lakini mara nyingi hutokea wakati unazo
Wakati wa dumba kali saa moja shuka utosini
Na kujifanya unawaza mambo mengi ya ofisini
Pitia pitia night kali mitaa ya Kinondoni
Kina dada poa nusu uchi fegi mdomoni
Na kama una gari watajazana madirishani wee
Mpaka ukose hewa wote wanataka hisani
Kwenye madaladala kuibiwa ni kawaida
Vaa cheni shingoni, saa mkononi utoe faida
Wacha dirisha wazi kisha ukatize Manzese
Ili uwape mateja mtaji waende chimbo wakatese
Rudi Mwananyamala oh! Mateja kibao
Katiza saa moja moja uone roba za mbao
Utaona kama mtoa roho yuko karibu yako
Ni kheri utoe chochote ili uokoe nafsi yako
CHORUS:
Bongo eh
Bongo Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Bongo Dares Salaam
Kaa chonjo eh
Ndani ya Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Ndani ya Dares Salaam
VERSE 2:
Bongo ya sasa sio ya mwaka 47
Mpaka bibi vizee sasa wanafanya ukahaba
Sijui niseme nini ili muweze kunielewa
Na sijui nifanye nini nisaidie wanaoonewa
Hakuna heshima, ni vurugu mechi kwenye jamii
Hakuna utii wala mafunzo ya manabii
Na wezi wa mfukoni wanachomwa moto kinyama
Mwingine hajaiba kapewa kesi kwa uhasama
Nani atakae jua na sheria ipo mikononi?!
Watu wa Bongo mbona hamna utu moyoni
Vijana wamejibana wapate mtaji wa biashara
Nawaita machinga ingawa sio wote kutoka Mtwara
Mbaya kuliko vyote mnapovunja vibanda vyao
Wengine walikuwa wezi, je warudie zama zao?
Ni mshike mshike sometime ni vita na mapolisi
Wao na sisi, rungu na pingu kama ibilisi
Huku kwetu uswahilini ni mambo ya kila siku
Na ni kama kuibiwa cheni kwenye ngoma za mchiriku
Wabongo wanapenda sana starehe kuliko kazi
Wanatamani wangezaliwa Blue Nay wamwage radhi
Masista duu wa Bongo wanazidi kupanda chati
Huwezi kujua yupi wa Kigogo, yupi wa Masaki
Mablaza majina yao ya asili hawayataki
Bitoz Nyangema anataka aitwe Tupac!
Ni burudani tosha, hivyo ni vijimambo tu
Wabongo tuna title kubwa lakini hatuna kitu
Unaujua mstakabari wa ma-superstar wa Bongo?
Lazma ufunzwe chuo kikuu cha mbwembwe za uongo
City center, ofisi ni mtu aliposimama
Hata muhuri wa ikulu unapata haina gharama
Ngoma inakuwa nzito mnapokutana matapeli
Akili kumkito ukilemaa umeachwa ferry
Aliyeuziwa cheni katoa hela bandia
Aliyepokea hela nae kauza cheni ya bandia
Tuliozoea jiji tunasema ngoma droo
Na una-set mambo mengine yaende kwenye mtandao
CHORUS:
Bongo eh
Bongo Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Bongo Dares Salaam
Kaa chonjo eh
Ndani ya Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Ndani ya Dares Salaam
VERSE 3
Katikati ya jiji hata usikiri dili haziji
Na ukitaka ku-win Bongo cheza dili na wale magwiji
Naona vijana wa Bongo wanapenda safari kafiri
Hata mkoba wanategua kitendawili
Safari bado ni ngumu jamani msiende kwa nguvu ya ndumba
Ujinga sumu acha Mwenyezi awahukumu
Changa uchange uende kiwanja unachotaka
Funga mkanda, fungua mabano unavyotaka
Maskani Kimara, watu kila siku mamtoni
Jonas Kiwia wasalimie Washington
Ukiweza pita Texas mpe hi Chief Son
Na mkumbushe uzushi wa Bongo Dar es Salaam
Sinza ya leo, kila baada ya nyumba bar
Na zote zinajaa, hapo ndipo utakaposhangaa
Na kwenye night club ni lundo la kaka poa
Huwezi ukaamini jinsi walivyojipodoa
Upinzani wa jadi Bongo haupo Simba na Yanga
Matonya na Makamba, na Sitte na wamachinga
Na kali kuliko zote upinzani konda na denti
Wanaposhika mashati tu denti anapoketi
Hakuna mnyonge, wala anayekubali kushindwa
Ngoma ngoroigwa na wote wanataka ubingwa
Na watu wana magari mpaka ya milioni 200
Kwa mbongo wa kawaida baiskeli kitendawili
Wasioamini ni wale wenzangu na mimi
Mlio na imani iliyopo juu mngoje chini
Mtangoja milele, na mtakufa bila kelele
Kama walivyokufa wafuasi wa Kibwetele
Ndani ya Bongo!
CHORUS:
Bongo eh
Bongo Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Bongo Dares Salaam
Kaa chonjo eh
Ndani ya Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Ndani ya Dares Salaam
Bongo eh
Bongo Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Bongo Dares Salaam
Kaa chonjo eh
Ndani ya Dares Salaam
Wasanii wa miaka hii wa hovyo sanaSiku izu utaskia nakuwa haraka kama nakula mbolea mara mwingine utaskia shipupy shipupy
Zote za prof jizz ni kali sana ref zile series ya ndiyo mzee
Saivi bongo flava ni singeli ni maajabu ya dunia
Profesa alikuwa anatoa hits song za uhakika
Kama unapata moja kwa nini usipate na mia,Chifu hiyo ni ngoma bora ya wakati wote ya collabo katika Bongo hip hop. Humo vichwa vilitulizwa vikaandika mashairi ya kina sana
Kuna hii punch line ya Jay huwa lazima ije akilini kila mara nikisia mtu anautaja huo wimbo
Wanakwenda hatua mbili, wanarudi kumi na kujipongeza,
Bila kuzingatia hatua nane walizopotеza,
Hao ni mafukara wa akili zao’ na uwezo wao
Kama unapata moja kwa nini usipate na mia,
Hii inawezekana kwa wote malio na nia,
Yeah hit songs zake mpaka leo zinaishi
Hapana vyote chorus na mistari ilisimamaHuu wimbo ulibebwa zaidi na kiitikio
Nafikiri aliyeanza ni Mr IIAlianza
Prof Jay ft Jide - Bongo Dar es Salaam
Jay Z ft Alicia Keys - Empire state of mind (New York)
Prof Jay ft Simple X & Sos B - Piga Makofi
Busta Rhymes - Make it clap
Sasa hivi naona yuko poa
Ile ngoma ni ya BaloziNafikiri aliyeanza ni Mr II
Hapo unaongelea series yenye uhalisia wa maisha ya kiafrika kwenye uongoziJay ana kipaji sana:
Ndiyo mzee Kikao cha dharura Nang'atukaUmeona huo ni mwendelezo wenye idea moja inayomhusu mwanasiasa aliyepewa dhamana baada ya kampeni na kushinda (ndiyo mzee)
Akaja akakosolewa na wanachi kwa kutotimiza ahadi zake alizotoa kwenye kampeni (kikao cha dharura)
Mambo yamekuwa magumu anaachana na siasa baada ya kuwa na kipindi cha utawala mbovu (nang'atuka)