TBT: "Bongo Dar es Salaam" hii ngoma Prof Jay alikuwa mbele ya wakati sana. Respect legend

Jay alikua mbele sana ya muda. Binafsi niliumia sana kusikia jamaa anaumwa very serious.

Vijana wa leo hawawezi kuelewa jitihada na miiko waliyovunja kina Jay hadi kuuleta huu muziki wa sasa na kuufanya ueleweke kwa watanzania.

Jamaa walilazimika kutumia akili kubwa sana kuja na ngoma kali sana zinazoishi muda mrefu ili kujijenga kijamii.

Albamu ya Machozi,Jasho na Damu ndio Albamu yangu bora toka Muziki wa Bongo Flava uanze Tanzania. Ngoma kama Bongo Dar es Salaam, Ndio Mzee, Niamini, Tathmini, Jina langu, ni ngoma ambazo Jay alitumia akili kubwa sana. Haipiti siku sijasikiliza ngoma mojawapo hapo.
 
Zote za prof jizz ni kali sana ref zile series ya ndiyo mzee
 
Jamaa walilazimika kutumia akili kubwa sana kuja na ngoma kali sana zinazoishi muda mrefu ili kujijenga kijamii.
Walifanya kazi kubwa sana hakuna leo wasanii wa kuumiza vichwa kama hawa wakongwe ​
 
Saivi bongo flava ni singeli ni maajabu ya dunia
 
Zote za prof jizz ni kali sana ref zile series ya ndiyo mzee
Jay ana kipaji sana:​
  • Ndiyo mzee​
  • Kikao cha dharura​
  • Nang'atuka​
Umeona huo ni mwendelezo wenye idea moja inayomhusu mwanasiasa aliyepewa dhamana baada ya kampeni na kushinda (ndiyo mzee)

Akaja akakosolewa na wanachi kwa kutotimiza ahadi zake alizotoa kwenye kampeni (kikao cha dharura)

Mambo yamekuwa magumu anaachana na siasa baada ya kuwa na kipindi cha utawala mbovu (nang'atuka)
​
 
Kama unapata moja kwa nini usipate na mia,
Hii inawezekana kwa wote walio na nia,
 
Alianza

Prof Jay ft Jide - Bongo Dar es Salaam

Jay Z ft Alicia Keys - Empire state of mind (New York)

Prof Jay ft Simple X & Sos B - Piga Makofi

Busta Rhymes - Make it clap

Sasa hivi naona yuko poa
​
Nafikiri aliyeanza ni Mr II
 
Hapo unaongelea series yenye uhalisia wa maisha ya kiafrika kwenye uongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…