TBT: Kati ya P Funk, Mikka Mwamba, Master J na Bony Luv, Mtayarishaji gani alikuvutia kwenye kazi zake enzi hizo?

Wote wakali ila Mika alikuwa Jini jamaa alikuwa anachafua kila mdundo kuanzia Hiphop, Dansi, bolingo mpaka Segere sijafuatilia tu vizuri nahisi hata Kwaya ashawahi kufumua


Mika Mwamba ni habari nyingine kabisa
 
Kipindi hicho mziki ulikuwa mziki. Yuko wapi mwamba

Said Comorien ?​

 
P funk ukiachilia kuwalazimisha wasanii walioenda studio kwake kutoa ngoma kuvuta mibangi alikuwa vizuri na beat nzuri zenye vina haswa..
 
I wonder MwanaFA hadi sasa haja-show up recognition na appreciation kwa Bon luv hadi sasa akiwa kwenye top position ya sanaa Tanzania. Wisely alitakiwa amefanya hivi mapema sana. Bon luv is a hero kwenye Tasnia ya muzik Bongo, he better should be cognized kbl ya kuanza kutamka ikiwa hatunae! I repect Bon, i respect Kusaga and Clouds Media kwa airtime and recignition of all gud thing kwenye Bongo!
Binafsi kuna watu wawili ambao whatever wanafanya kazi i won't regrect kuungana nao; Bon luv 2 John Dillinga. Wanao mchango mkubwa kwa tasnia hii ya bongo fleva.
 
Mzee wa Tehran inaonekana haya madude unayapata vyema sana.

Jamaa walikuwa vipaji asee.
 
Nashindwa kusema yupi mkali kutokana kwamba Kila producer alikua ana ladha na midundo unique, lakini nikisikiliza Ngoma kama Kama unataka demu- Jay Moe, Nini mnataka- Pig Black, naishia kusema P funky ni Bora kuliko wote.. jamaa alikua mtu sana na ndo maana kura nyingi zinamwangukia yeye...
 
Kila jambo nalofanya unaona Halifai baby gal, Baby nifanyeje,nifanye jambo gani uelewe nifanye jambo gani nikulizishe.....aisee Mika Mwamba alikuwa mwamba kwelikweli vinanda vilivyotumika ktk intro siyo mchezo
Bila shaka unaiongelea ile remix (R&B version) maana mixing ya mle hata leo hii bado ni ya kisasa..yaani ilikua ahead of time
 
Kila mmoja alinivutia kwa ngoma fulani.
Pfunk ngoma kibao za akina jay mo, nature n.k
Bon luv ngoma ya mabinti famu damu na nyingi kibao
Master jay ngoma kibao za mike t na nyingine kibao.
Halafu mkuu ngoma ya raha tu aligonga marehemu complex
Hapana mkuu, ngoma ya AY Raha Tu aliifanya Mikka Mwamba na ikawa kwenye compilation ya track za Mikka Mwamba kama Mdundiko (Mambo Jambo), Usiniache (D Knob ft Mez B), Fikiria (Mez B).

Kwenye Raha tu AY aliimba peke yake lakini baadae akafanya Raha tu Remix kwa P Funk (Bongo records) ndio akaimba na Complex. Complex production rasmi alianza mwaka 2005 mwanzoni kwa kufanya ngoma kama Nyeti (wagosi wa kaya), unanitega (FA ft Noorah), Siku nzuri (Dan Msimamo), Nilikaona Mwaka jana (Soggy)

Hii ni Raha Tu Original (Mikka) ๐Ÿ‘‡๐Ÿฟ

View: https://youtu.be/Hw_rp0xIoz0?si=3DGJsldau1KBhuMp
Hii ni Raha tu Remix (P Funk)๐Ÿ‘‡๐Ÿฟ

View: https://youtu.be/tbX02ku4JLM?si=owPGkeyMNvTLrNMa
 
Huyu mzungu (Mika) aliwezaje kutengeneza ngoma ya asili Maria Salome, yani mule zinapigwa ngoma za asili kabisa au maisha yake kabla alizaliwa mzaramo?
Jamaa unaambiwa alikua hajui hata Kiswahili vizuri, yeye anakusikiliza na anajua nini aandae kikufae. Ikiwa nyimbo ya kusikitika inatoka ya kusikitika kweli kama vile Kamanda (Daz Nundaz), Mkiwa (K Sal) na ikiwa ya ku-party inakua inaamsha kwelikweli ndio kama Enno Mic (Ziggy D), Mpenzi (Dudubaya), Chacha (ManDojo na Domo Kaya). Alivyorudi 2003 alitengeneza ile ngoma ya Mambo Jambo - tumerudi tena kaeni mkao wa kula, ni kiasili flani.

Hata baby gal original ya Mad Ice alitumia marimba instrument na ngoma ikawa na uasili asili hivi
 
Mkuu just kuweka record straignt, umesema kuwa complex alianza production mwaka 2005, ina maana alianza production mwaka huo huo aliofariki. Historia fupi ya complex :
Miaka 19 imepita tangu kifo chao Simon sai au complex na Vivian tilya au viv.wawili hawa mmoja alikuwa producer na mwanamziki hapa namzungumzia complex aliyekuwa katika studio za aigies record na baadae kuhamia backyard record wakati huo Vivian alikuwa mtangazaji wa clouds f.m. wawili hawa walikutanishwa na A.y .kisa Cha kukutana nakuwa wapenzi Kiko hiv Vivian alifahamiana na A.y iringa kipind A.y anasoma ifunda na Vivian alikuwa anasoma mkwawa..A.y baada ya school alikuja kukutana na Vivian Arusha alipoenda kwenye show akamshawish Vivian kwa muonekano wake awe mtangazaji. Vivian akaelewa mchongo akakutanishwa na Gardener G habash pale clouds akapewa mchongo wa utangazaji.simon sai a.k.a complex alikuwa anafanya kazi na A.y Kuna ngoma walishirikishana kiufupi walikuwa maswahiba wakubwa baada ya kufahamiana.simon sai a.k. complex akamuona Vivian pale clouds kupitia A.Y akatokea kumpenda vivian.kwakuwa Vivian na complex wote walikuwa marafiki wa A.Y basi A.y akarahisisha wawili hawa kuwa karibu. Baada ya hapo kilichofuata nikuibuka kwa penzi zito kati ya complex na viv..mahusihano Yao yalianza miaka ya 2000 kufika 2005 august 21
 
Yeah, kwa maana ya yeye kuwa produsa kabisa na ngoma kuachiwa kwa credits zake ilikua ni hiyo 2005, alidumu kwa muda mfupi sana, na alikuwa anakuja kwa kasi sana.

Lakini inamaanisha kuwa alikuwa anajifunza na kugusa gusa kazi za wasanii kwa miaka ya nyuma kabla ya yeye kukabidhiwa jiko rasmi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ