Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Watanzania, tufike mahali tujiulize swali hli dogo tu:
Mikopo ya mitandaoni hutolewa kwa wateja kutumiwa hela kwenye simu zao na zaidi marejesho hutumwa kwa haya makampuni kwa kutumia lipa namba za mitandao ya simu. Sasa kama mpaka wanakuwa wamesajili lipa namba kwenye menu ya mitandao ya simu, TCRA wanashindwa nini kuagiza makampuni ya simu kusitisha maramoja usajili wa lipa namba za haya makampuni kama kweli wana dhamira ya dhati ya kudhibiti hii biashara inayofanywa kihuni na baadhi ya makampuni?
Mpaka kusajili namba ya kufanyia malipo maarufu kama "namba ya kampuni" , ni lazima utatakiwa kuwa na viambatanisho maalumu, na kama sikosei, utatakiwa kuwa na leseni ya biashara, leseni ya BOT, cheti kutoka BRELA, n.k pamoja na kutoa taarifa zingine kama anuani ya makazi, n.k.
Kwa mtazamo wangu, TCRA, kama regulator, kwa kushirikiana na BOT na makampuni ya simu, wangeweza kabisa kudhibiti wanaofanya hii biashara ya kukopesha mitandaoni bila kufuata taratibu, ila nachokiona hiyo dhamira haipo na ndio maana hii biashara haramu inazidi tu kushamiri humu nchini.
Je, tukisema kwasababu serikali inapata kodi na makampuni ya simu nayo yanapata faida kwa kila transaction inayofanyika na ndio maana hatua hazichukuliwa, tutakuwa tunakosea?
Nato wito kwa waandishi wa habari na hata wabunge wahoji maswali specific kama haya kwa TRCA, BOT na makampuni ya simu kwasababu haiwezekani watu wafanye biashara haramu kwa kutumia mitandao ya simu inayosimamiwa na kudhibitiwa na serikali halafu serikali ikashindwa kuwabaini hawa watu. Haingii akilini hata kidogo.
TCRA, kama sheria na kanuni zinawabana katika kudhibiti haya makampuni, kwanini hamchukui hatua za kubadili sheria na kanuzi au kuomba kutungwa kwa sheria/kanuni mpya zitazowawezesha kukabiliana na haya mapungufu kama wanavyofanya BOT kwa kutoa miongozi mipya kila wakati?
Tuache kudanganyana kabisa kuhusu haya mambo.
www.jamiiforums.com

Mikopo ya mitandaoni lawama zinawahusu pia TCRA, msikwepe
Nimeskia redioni TCRA wanasema hawahusiki na hiki kinachoendelea kwenye mikopo mitandaoni. TCRA mnaweza kuwa hamuhusiki kweli ila na nyie pia mmezembea sana kama wenzenu BOT licha ya makelele mengi kuhusu hawa mikopo mitandaoni ambao wengi hawajajisajili na wala hawana physical address. kwanza...