TCRA an instrument of repression? Chombo cha kukanyaga haki za uhuru wa habari?

TCRA an instrument of repression? Chombo cha kukanyaga haki za uhuru wa habari?

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Mimi si mwanasiasa.
Mimi si mpenzi wau mfuasi wa Lissu(actually nimekuwa nikipinga mambo mengi ya Lissu na maneno yake)
Mimi ni mtanzania huru chini ya katiba ya nchi ya Tanzania.

Kinachonishangaza ni juhudi za watu fulani ndani ya serikali kukiuka uhuru wa Mtanzania wa kawaida kupata habari na kutoa maoni yake juu ya habari hizo.

Majuzi TCRA wamekipiga fine kituo kimoja cha habari kwa kutekeleza haki hiyi ya mwananchi KUJULISHWA kinachoendelea nchini.
Kosa walilofanya "eti" ni kurusha matangazo ya redio BBC ambayo kwa njia moja au nyingine kilirusha habari za Tundu Lissu.
Kama nilivyosema Tundu Lisuu huwa sikubaliani naye mara nyingi, lakini haki ya kusikia anachosema ni uhuru wa wananchi.
Sasa TCRA kutumika kuwa agent wa kuzima haki ya kupata habari , huu ni udhifu mkubwa sana.
TCRA inaanza kutumika kama chombo cha kuzuia haki za msingi za mwananchi.
Nafikiri matumizi ya chombo hiki kana kunavyotumika sasa, sivyo kilivyotarajiwa na wananchi.
Chombo cha kitaaam kinatumika ndivyo sivyo, na sasa kinaaza kuvuna chuki za wananchi.
Tujizuie chonde chonde kukiharibu ili kitumike kama kilivyotarajiwa.

Uhuru wa kupata habari umeainishwa katika Katiba kifungu cha 18(b) kama nilvyo nukuu:

The Right to Freedom of Conscience Freedom of expression

18. Every person -
(a) has a freedom of opinion and expression of his ideas; Act No.1 of 2005 Art.6
(b) has a right to seek, receive and, or disseminate information regardless of national boundaries;
(c) has the freedom to communicate and a freedom with protection from interference from his communication; and
(d) has a right to be informed at all times of various important events of life and activities of the people and also of issues of importance to the society.
 
Nawaomba wana CCM wenzangu , habari tunazo zipata na maoni wakati huu wa uchaguzi ziwe kipio cha uvumilivu!

Kutotaka kusikia mapungufu yako, mtu ni kukosa uvumilivu.
 
Nawaomba wana CCM wenzangu , habari tunazo zipata na maoni wakati huu wa uchaguzi ziwe kipio cha uvumilivu!
Kutotaka kusikia mapungufu yako, mtu ni kukosa uvumilivu.
Kukubali/kutokubali kukosolewa na kuzima vyombo ili wanaokukosoa ni vitu viwili tofauti.

Kuvizuia vyombo vingine vya habari ili wananchi wasisikie kile kinachoendelea duniani kidogo hili halijakaa sawa.
 
.... TCRA iliundwa kwa matarajio ingeziba gap la SHIHATA (watoto wa juzi wanaweza wasielewe) lakini matokeo ni kinyume kabisa na matarajio.
 
Upuuzi ukizidi kiwango hata hicho kidogo kizuri kinageuka ujinga mtupu
 
.... TCRA iliundwa kwa matarajio ingeziba gap la SHIHATA (watoto wa juzi wanaweza wasielewe) lakini matokeo ni kinyume kabisa na matarajio.
SHIHATA mkuu lilikuwa shirika la habari la serikali wakati TCRA ni mdhibiti na msajili wa vyombo vya habari na masafa.
 
Upuuzi ukizidi kiwango ata hicho kidogo kizuri kinageuka ujinga mtupu.
Ni kweli TCRA sasa ni POLISI wa habari. Tena si polisi mzuri basi maana anafanya kile kinachompendeza aliye muagiza.
Imesha kuwa idara ya siasa.
 
Ni kweli TCRA sasa ni POLISI wa habari. Tena si polisi mzuri basi maana anafanya kile kinachompendeza aliye muagiza.
Imesha kuwa idara ya siasa.
TCRA kwa sasa hawako vizuri.
Malalamiko kila kona kwa kutumiwa vibaya.

Sasa vipindi vya BBC na redio za nje ni shida kupata.

Isiwe kuwa ndio mpango wa kukata mawasiliano ya internet inasukwa sasa.
 
TCRA kwa sasa hawako vizuri.
Malalamiko kila kona kwa kutumiwa vibaya.
Sasa vipindi vya BBC na redio za nje ni shida kupata.
Isiwe kuwa ndio mpango wa kukata mawasiliano ya internet inasukwa sasa.
Kidhibiti matangazo ya BBC au VOA na redio nyingine za nje ni kukiuka uhuru wa habari.
 
Rais ajaye ana Mambo mengi yakubadilisha kwa nchi maana sikuhizi maoni ya wananchi hayaheshimiwi Ila hisia za mtu mmoja tu

TCRA imekuwa sehemu ya kukomoa vyombo vya habari, pia kunyima Uhuru wa habari kupangia watu waangalie TBC tu na habari fulani. Inasikitisha nchi yetu kuanza kurudi miaka ya themanini huko
 
Government apparatus are tools of oppression!

Any oppression, mass killings, ethnic cleansings, etc are always government connected!

Citizens as human beings generally are peaceful good people when left alone....

Government is always a problem!
 
Government apparatus are tools of oppression!

Any oppression,mass killings,ethnic cleansings,etc are always government connected!

Citizens as human beings generally are peaceful good people when left alone....

Government is always a problem!
And if the Government is overdoing it in controlling news access, it turns the people against it.
Somebody should realise this.
 
Ni wajinga wa kutupa kosa lilelile Abood fm imepewa onyo lakini radio free Africa imepigwa faini ,maajabu ya Rahman.
 
Back
Top Bottom