TCRA haioni hawa matapeli mitandaoni wanaotumia majina ya watu maarufu kujinadi kuwa wanatoa mikopo?

TCRA haioni hawa matapeli mitandaoni wanaotumia majina ya watu maarufu kujinadi kuwa wanatoa mikopo?

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Hii inanishangaza sana. Watu wanatoa wapi ujasiri wa hadi kulipia kabisa matangazo Insta na Facebook kunadi utapeli wao huku TCRA ikiwepo? Ninashangaa sana. Nimeona kuna matapeli yanatumia majina ya Mo Dewji, Spika Mstaafu Tulia na Lady Jay Dee kudai wanatoa mikopo huku wakijua kabisa ni uongo. TCRA haiwaoni?

Mimi huwa ninafurahi sana wajinga wasio na akili wanapopigwa na hawa matapeli kwasababu ya tamaa zao za kutaka urahisi. Imagine kampuni inadai ina kibali cha katibu wa bunge cha kutoa mikopo ila wajinga hawashtuki na kujiuliza katibu wa bunge anahusikaje na mambo ya mikopo? Mbaya zaidi maandishi yameandikwa kwa kiswahili kibovu mno. Nimeweka picha ya kitambulisho feki cha Mo na idhini ya katibu wa Bunge. Nchi bado ina wajinga wengi mno.

Mimi nimetafakari na kuona bado wanaopigwa ni ndugu zetu lazima tufanye jambo kuwasaidia. Utakuta mtu ni muumini wa Mwamposa, mwanachama wa CHADEMA halafu bado anaishia kupigwa na haya matapeli. Yaani badala ya kumhurumia tayari kwamba yuko matatizoni kwa kuuziwa udongo na kuchangishwa kihuni tonetone wao wanamtapeli tena hela.

Ninawasihi watanzania wenzangu tujiepushe na hii mikopo ya kihuni. Kama una shida ya mkopo nenda kwenye taasisi iliyosajiliwa ofisini kwao. Achana na hizi za mtandaoni. Pia ninaisihi TCRA ichukue hatua kali kwa hawa wahuni.
 

Attachments

  • FB_IMG_1790781427704.jpg
    FB_IMG_1790781427704.jpg
    56.2 KB · Views: 13
Duh,
Na hao ambao majina yao yanatumiwa kutapelia kwa nini hawachukui hatua kuzuia?

Wengine wa kulaumiwa ni makampuni ya simu ambayo namba zao zinahusika, policcm, nk..
 
TCRA naona hawahusiki na utapeli kwa Tanzania wangekua wanahusika wangekamatwa hao jamaa baada ya kutuma tu matangazo yao ya kitapeli kila kukicha maana unaona mpaka wafanyakazi wa TCRA wanapata meseji ya tuma hela kwenye namba hii ila nao wanabaki kucheka tu.
 
Shida kubwa ipo Kwa Benki kuu ya Tanzania (BOT). Hawa, kisheria, ndiyo wanaotoa leseni za kampuni zote zinazotoa huduma za kifedha (ikiwemo mikopo) nchini Tanzania.
Kwa jukumu hili la kutoa leseni pia ndiyo wasimamizi wa taasisi hizi.
Cha kushangaza ukiingia ktk wavuti (website) wa BOT wameweka orodha ya taasisi/ kampuni zinazotoa mikopo bila kuwa na usajili wa BOT. Ni Kwa nini sasa hizi kampuni zinaendelea kufanya Biashara bila usajili wa BOT? Ni uzembe, kupuuza sheria au na wao ni wadau wa hizo kampuni? Je, wanasubiri maelekezo kutoka juu?
 
Back
Top Bottom