Shida kubwa ipo Kwa Benki kuu ya Tanzania (BOT). Hawa, kisheria, ndiyo wanaotoa leseni za kampuni zote zinazotoa huduma za kifedha (ikiwemo mikopo) nchini Tanzania.
Kwa jukumu hili la kutoa leseni pia ndiyo wasimamizi wa taasisi hizi.
Cha kushangaza ukiingia ktk wavuti (website) wa BOT wameweka orodha ya taasisi/ kampuni zinazotoa mikopo bila kuwa na usajili wa BOT. Ni Kwa nini sasa hizi kampuni zinaendelea kufanya Biashara bila usajili wa BOT? Ni uzembe, kupuuza sheria au na wao ni wadau wa hizo kampuni? Je, wanasubiri maelekezo kutoka juu?