TCRA: Hatujakataza matumizi ya VPN bali ni kusajili na kutoa taarifa ya matumizi ya VPN

TCRA: Hatujakataza matumizi ya VPN bali ni kusajili na kutoa taarifa ya matumizi ya VPN

Hizo nchi za mfano Sasa ! Mh hhhhh.....Uturuki,India,China,Belarus ,Misri ...na si ajabu pia Kuna Somalia,Yemen,Syria,Gaza na mamaLao Afghanistan.
 
Ukienda kujisajili huko inakuwa hakuna maana tena ya kutumia VPN.

Inakuwa sawa na kujificha mahali huku unaimba!
 
Daah bora angekaa kimya tu hakuna alichoongea hapo anazidi kuwapa hasira Wananchi mafuta wanapandisha hovyo bila kuweka mazingira yeyote mazuri kwa Wananchi leo wanasema tupeleke taarifa za simu tunazotumia baadae mtasema mnataka taarifa za Betri zote kwa kuw Somalia wamefanya hivyo...
 
View attachment 2783028

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia kwa Mkuu wake wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Rolf Kibaja imesema taarifa kwa Umma iliyotolewa juzi October 13,2023 haijakataza matumizi ya VPN kama baadhi ya Watu a"
Mwisho tutahitaji kujisajiri tukitaka kunongonezana. Nini maana ya VPN?
 
Bwana R.Kibaja yupo sahihi.

...Wapo wanaopotosha kuhusu utaratibu unaotakiwa kufuatwa. Sambamba, hakuna sehemu kwenye taarifa ya awali, inayodai "wanakataza" utumiaji wa VPN

Naunga mkono TCRA.
 
Kila siku hapa duniani watu wanapasua vichwa kubuni na kuvumbua vitu vipya ili kurahisisha maisha ya mwanadamu, kadiri miaka inavyokwenda mbele ugunduzi na uvumbuzi huu unafanya maisha ya watu duniani kuwa rahisi zaidi kuliko zamani. Kuna tofauti kubwa sana maisha yalivyokuwa miaka 50 iliyopita na sasa. Tunapaswa tuzikimbilie na tuzikumbatie hizi fursa za ugunduzi na uvumbuzi wa teknolojia ili maisha yetu yawe rahisi na nchi na jamii nayo iendelee.

Jambo la ajabu na la kusikitisha ni kwamba kuna watu waliopewa dhamana hawalioni hili, badala yake wanawarudisha watu nyuma, wanawanyima maendeleo, ni kama vile wanataka watu waendelee kuishi kama miaka 50 iliyopita. Wanataka kudhibiti kila kitu, kwanini? Kwa faida nani?!

Nguvu kubwa inayotumika kudhibiti hizi fursa za kiteknolojia kwanini zisitumike kuboresha umeme, kuleta maji, na kuwaletea unafuu wa wananchi?
 
"Uturuki, India, Belarus, Misri, China"

Hapo kwenye Belarus na China mnazichukuliaje hizo nchi?
 
Back
Top Bottom