Kila siku hapa duniani watu wanapasua vichwa kubuni na kuvumbua vitu vipya ili kurahisisha maisha ya mwanadamu, kadiri miaka inavyokwenda mbele ugunduzi na uvumbuzi huu unafanya maisha ya watu duniani kuwa rahisi zaidi kuliko zamani. Kuna tofauti kubwa sana maisha yalivyokuwa miaka 50 iliyopita na sasa. Tunapaswa tuzikimbilie na tuzikumbatie hizi fursa za ugunduzi na uvumbuzi wa teknolojia ili maisha yetu yawe rahisi na nchi na jamii nayo iendelee.
Jambo la ajabu na la kusikitisha ni kwamba kuna watu waliopewa dhamana hawalioni hili, badala yake wanawarudisha watu nyuma, wanawanyima maendeleo, ni kama vile wanataka watu waendelee kuishi kama miaka 50 iliyopita. Wanataka kudhibiti kila kitu, kwanini? Kwa faida nani?!
Nguvu kubwa inayotumika kudhibiti hizi fursa za kiteknolojia kwanini zisitumike kuboresha umeme, kuleta maji, na kuwaletea unafuu wa wananchi?