Nchi yetu na nyingi za ulimwengu wa tatu zina tatizo kubwa la kuruhusu jambo lililo kinyume na sheria ama uhuni tu kuendelea kwa muda huku taasisi zenye kazi ya kuzuia uhuni huo kukaa kimya.
Unaweza kusema huwezi kutapeliwa, lakini hiyo haina maana kuwa kinachoendelea kiendelee tu.
Nakumbuka tarehe 9 Mei 2022 majira ya saa 2.50 usiku nilipopokea ilikuwa simu ya ndugu yangu lakini alitumia namba ya mtu mwingine akiomba kiasi fulani cha pesa ili afanyiwe kipimo siku ya pili asubuhi (huyu alikuwa mgonjwa amelazwa katika hospitali fulani), katika mazungumzo nilimuuliza hiyo pesa nitume kwenye namba hii? akasema ndio.
Uzuri nilikuwa na hicho kiasi hivyo skupoteza muda, nikafanya muamala. Nikapiga kumueleza kuwa nimeshafanya muamala, naye akathibitisha kupokea.
Dakika chache baadaye ikaingia meseji kutoka namba 0733 584 129 iliyosomeka
''Nitumie tu kwenye namba hii 0716 135 528 Jina ni PAULO MAEMBE''
Hapa nikatafakari sana, kutapeliwa ni rahisi sana kwa sababu ya ''coincidence'', yaani kama ningekuwa sijatuma ile hela kwa ndugu yangu kulikuwa na nafasi kubwa sana kwa mimi kutuma ile hela kwa sababu ya mfuatano wa matukio na uharaka wa pesa husika.
Kwa kuwa nilikuwa na muda na kwa kuwa ni jambo rahisi kufanya uchunguzi mdogo, nikaamua kuanza kumtafuta huyu mtu anayeitwa Paulo Maembe.
Katika ulimwengu wa kidijitali, kupata taarifa ni jambo rahisi sana. Na wengi wetu tunaacha ''digital prints'' kwenye mitandao ya kijamii.
Kupitia ''search engine'' jina la Paulo Maembe likatokea mara kadhaa, nikaanza kumtafuta kwenye mitandao, baada ya siku chache nikapata mpaka namba halisi ya simu na mahali anapoishi.
Baada ya mazungumzo nikagundua kuwa namba yake imesajiliwa mara kadhaa na yeye mwenyewe hajui. Kwa wepesi tuliweza kuthibitisha mpaka kijana aliyemsajilia line ya simu ambaye kwa makusudi alisajili namba za ziada kwa sababu hizi za utapeli.
Zoezi la yeye kuthibitiisha namba zake likafanyika na hatimaye ile namba ya utapeli ikawa ipo ''deactivated''.
Mambo machache niliyogundua kuhusiana na huu utapeli wa ''tuma kwenye namba hii''
1. Vijana wengi wanaosajili namba nje ya ofisi husika za mitandao ya simu, huwa wanasajili namba nyingi unapoenda kusajili.
Wakati wanakwambia network inasumbua huku ukiwa umeshaweka finger print jua amesajili namba ya kwanza, anapokwambia embu turudie jua hapo inasajiliwa namba ya pili. Baada ya hapo anakupa namba moja huku ukiwa umebakisha namba nyingine mezani kwake ambayo yeye ataiuza kwa wanaohitaji hiyo namba.
Hizi namba zinanunuliwa na watu wengi haswa hao matapeli lakini hata ambao sio matapeli wanapotaka kuficha identity zao.
Kwa mujibu wa hawa vijana hizi namba huuzwa kati ya 30,000 - 50,000/-
Wengine wanaonunua namba hizi ni wageni wanaoishi hapa Tanzania hasa hawa wanaotoka nchi za Kiafrika.
2. Watu wengi hawana muda wa kujiridhisha namba ambazo zimesajiliwa kwa majina yao ( Namba ya Kitambulisho cha Taifa) , wengi wanatembea mjini hapa lakini kitambulisho chake kimetumika kusajili namba nyingi bila wao kujua na hawataki kujua.
3. Mfumo wa TCRA wa kuwasilisha malalamiko na mitandao ya simu sio rafiki sana. Maana inabidi mara nyingi uanzishe kesi polisi, na kama mjuavyo Watanganyika na masuala ya polisi. Wengi huamua kuacha tu huku wakisubiri tukio lingine la utapeli.
4. Watu wengi hatuna muda wa kutaka kujiridhisha kuhusu mtu tunayetaka kumtumia pesa, inawezekana una ahadi ya kumtumia pesa mtu, yaani ukipokea meseji ya hivi huchukui muda kutaka kuthibitisha. Ni vyema tuwe tunathibitisha.
View attachment 2239057View attachment 2239057