KERO TCRA, hawa matapeli wa “TUMA KWA NAMBA HII” tutaishi nao milele?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kuna shida, piah Kwa baadhi ya wasajili lain Wana Tabia ya kujifanya mtandao unasumbus mara baada ya mteja kuweka fingerprint, na kumtaka mteja arudie Tena kuweka kidole, na hapo kusajili lain nyingne pasipo mteja kufaham kma namba yake ya NIDA imesajili zaidi ya namba Moja, piah linapaswa lidhibitiwe hili
 
Juzikati hapa nilienda kwa wakala wa airtel money kuweka kiasi fulani cha pesa katika simu yangu, baada ya kutoka tu kwa wakala sikukaa hata lisaa nikaanza kupigiwa simu na watu wanaodai ni wahudumu wa wateja Airtel, mbaya zaidi wakawa wananipigia kwa kutumia laini za mitandao mingine tofauti 😅. Hapa nachelea kusema kabisa kuna namna hawa watu wanashirikiana kujua nani ana pesa na nani hana, pia mara nyingi kwann laini za TTCL ndio zinatumika zaidi kutuma hizo sms? 🤔
 
Hii ni changamoto inayotusumbuwa kwa kiwango kikubwa sana, ukiwa una fanya miamala miamala ya simu mara kwa mara , au ukiwa unatunza pesa zako kwenye simu kwa hizi pesa pesa.

Ukiachana na hizi messages wanazotutumia kuna mda wanafanya hadi direct transfers kutoka line yako kwenda kwenye Bank Account fulani.

Ukianza kufuatilia tu unakuta hata polisi wenyewe wana anza kuku katisha tamaa au utafute mtu wa nje kwa gharama zako binafsi akufuatilie kumtafuta muhisika wa apo na bado uta ambiwa akuna assurance ya kupata ulichopteza kwa 100% zaidi utaongeza gharama za ufuatiliaji.

Huu ni mtando sio mdogo na wanahusika na huu wizi wengi.

Kikubwa cha kushauriana tu ni kwamba tuwe tunatumia sana Bank kufanya miamala yetu ya kifedha na kutoweka kiasi kikubwa cha fedha kwenye hizi simu pesa pesa kwenye laini.

Mabenki mengi yapo serious na Brand zao.

Tuweni makini sana maaana hawa watu wanarudisha sana watu nyuma
 

Swali ni je kwa nini system ya mitandao ya simu isikatae kusajili tena namba iliyosajiliwa na kuwa active? Au kwanini tcra au kampuni za simu zisifute namba zilizojirudia usajili ibaki namba moja ya mteja kisha mteja atakapoona mabadiliko yoyote asiyoyaelewa basi aende kwa wakala ku-claim namba yake? Hii nafkiri itakomesha. System bado haijatumika vizuri.

Unless otherwise makampuni ya simu yanashirikiana na hao matapeli kwenye kutapeli wananchi.
 
Sijaisoma mada yote, lakini narudia tena kusema, cha ajabu siku hizi matapeli wanatumia namba za TTCL (Kampuni ya Serikali) kupiga na kutuma ujumbe mfupi.
 
Jengo lao kubwa maofisi mengi lakini hamna wanachokifanya.
 
Kuna mapungufu mengi ya kitaalamu na ubunifu TCRA ni kama vile hawapo,
 
kweli kabisa mkuu
 
Mara ya kwanza tuli register kwa kitambulisho, then wakasema biometrics, tukapiga foleni ku register. Lakini utapeli unaendelea. Next tutaambiwa ku register na retinal scan. Hizi taasisi kama TCRA naona mambo yamewashinda kabisa.
 
Tangu mhandisi James Kilaba aondolewe Pala TCRA, mambo yameenda hovyo sana, yaani TCRA imekuwa kama ttcl, ni utapeli mtupu
 
Ukifuatilia utaona hizi sms zinakufikia sana pale either ukiwa na hela kwenye simu au ukiwa umefanya miamala kadhaa which means mitandao ya simu kuna watu wasio waaminifu wanauza taarifa za wateja.
Kuna ukweli kwa hili
 
Nawatukanaga wakikata nawapigia Tena mpk wazime simu shenzi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…