Mojawapo ni Star Tv pia YouTube channels zote na magazeti. Vyombo vingine vipelekewe taarifa ya tahadhari, hasa vinavyorusha matangazo ya wachungaji wahuni wahuni
Mawazo yako ni ya HOFU isiyokuwepo na basically siku zote mwenye HOFU/WOGA juu ya jambo fulani, huyo ndiye mwenye shida na uhitaji wa kusaidiwa...
Na shida yenu nadhani ni njia aliyotumia kurusha tuhuma zake kuwa siyo mliyotarajia. Lakini ukweli ni kuwa maelfu ya watu wanaulalamikia na kuutuhumu utawala wa serikali ya Magufuli kwa matendo maovu mengi sana ikiwemo mauaji. Sema hao ni waoga nà au hawana access ya media kama alivyofanya Nabii na Mtume Mwingira kulipua bomu hili. Lakini kumbuka pia Freeman Mbowe alishawahi kutoa madai kama haya pia...
On the other hand, mbona Nabii na Mtume Mwingira kasema hayo kwa uwazi mbele ya kila mtu kwenye kamera za TV akisikika na kuonekana duniani kote? Shida ni nini kwani? Kasema uongo? How do you know kuwa ni uongo?
HAPANA!!... Ni wazi kuwa jambo hilo ni la HAKIKA na KWELI na anaweza kuthibitisha bila shaka...
Ningekuelewa vyema kama ungetoa wazo la huyu Nabii na Mtume kuthibitisha madai yake katika mamlaka zinazohusika hususani mahakama...
Sasa mnataka watu wasitoe madukuduku ya madhira na maumivu yao waliyotendewa na watu wengine? Je, una maana hutaki Nabii spate kusaidiwa kurejesha mali zake anazosema ziliharibiwa na serikali...
NDIYO, lazima mshituke kwa sababu inayotuhumiwa ni SERIKALI kupora au kuharibu mali ya wananchi inayowaongoza
Ofcoz si jambo la kawaida kwa kiongozi/viongozi wa serikali kutuhumiwa kuhusika kwenye UOVU na uharibifu na uporaji wa mali za RAIA wake...
Lakini ni LAZIMA watu waseme mabaya na mazuri ili;
1. Tuyalinde na kuyaenzi mazuri yote ya viongozi wa serikali zetu zote zilizopita
2. Kuyarekebisha na kuacha kabisa mabaya yote yaliyotendwa na viongozi wa serikali zilizopita na kwa kila tendo baya au ovu (ikibidi) hatua za kisheria zichukuliwe na adhabu zitolewe kwa kila aliyehusika ili kuwaonya na kuwa fundisho kwa viongozi wa serikali iliyopo na zile zitakazokuja huko mbeleni...
KWA HIYO, badala ya kuwa harsh & aggressive kwa watu wanaolalamika kuwa walinyanyaswa, kuonewa na kuporwa mali zao na utawala wa Rais aliyekwisha kufa Hayati Magufuli, tuwaache waseme na kama tuhuma/madai yana ukweli hatua zichukuliwe ikibidi wawe compensated na serikali yenyewe iliyotenda uovu huo...!!
Hapa ndipo ule umuhimu wa kuundwa kwa chombo yaani TUME YA MARIDHIANO na MAPATANO YA TAIFA unapokuja...