TCRA imeendesha kikao Kazi na Wadau wa sekta ya Mawasiliano Kanda ya Kati

TCRA imeendesha kikao Kazi na Wadau wa sekta ya Mawasiliano Kanda ya Kati

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
TCRA imeendesha kikao Kazi na Wadau wa sekta ya Mawasiliano Kanda ya Kati


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari, ameongoza kikao kazi baina ya TCRA na Wadau wa Sekta ya Mawasiliano Kanda ya Kati, kilichofanyika Mkoani Tabora, katika ukumbi wa Isike Mwanakiyungi uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, kujadili uboreshaji wa ufanisi wa Huduma za Mawasiliano nchini, Tarehe 29 Agosti, 2022.

Mkutano huo umehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Burian @batilda.burian aliyeambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Dkt. John Mboya.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Bakari aliambatana na Meneja wa TCRA Kanda ya Kati, Bw. Boniface Shoo, Mkurugenzi wa Idara ya Leseni na Ufuatiliaji - TCRA, Bw. John Daffa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Bi. Lucy Mbogoro pamoja na Watumishi wengine wa TCRA.
 

Attachments

  • IMG-20220829-WA0225.jpg
    IMG-20220829-WA0225.jpg
    78.1 KB · Views: 8
  • IMG-20220829-WA0223.jpg
    IMG-20220829-WA0223.jpg
    93.9 KB · Views: 8
  • IMG-20220829-WA0224.jpg
    IMG-20220829-WA0224.jpg
    56.7 KB · Views: 8
  • IMG-20220829-WA0226.jpg
    IMG-20220829-WA0226.jpg
    115.5 KB · Views: 9
  • IMG-20220829-WA0231.jpg
    IMG-20220829-WA0231.jpg
    88.3 KB · Views: 8
  • IMG-20220829-WA0229.jpg
    IMG-20220829-WA0229.jpg
    79.5 KB · Views: 7
  • IMG-20220829-WA0227.jpg
    IMG-20220829-WA0227.jpg
    51.8 KB · Views: 6
  • IMG-20220829-WA0228.jpg
    IMG-20220829-WA0228.jpg
    104.7 KB · Views: 6
  • IMG-20220829-WA0230.jpg
    IMG-20220829-WA0230.jpg
    98.7 KB · Views: 7
  • IMG-20220829-WA0233.jpg
    IMG-20220829-WA0233.jpg
    126 KB · Views: 6
  • IMG-20220829-WA0234.jpg
    IMG-20220829-WA0234.jpg
    131.5 KB · Views: 6
  • IMG-20220829-WA0235.jpg
    IMG-20220829-WA0235.jpg
    142 KB · Views: 6
Wana JK

Nimetimiza wajibu wangu kuleta taarifa binafsi baada ya kuridhika na uchunguzi nilioufanya juu ya uzembe wa TCRA na Wizara ya Mawasiliano na usimamizi wa makampuni yanayotoa huduma za mitandao.

Nilichofanya. Nilienda kwa vijana nikijifanya nimenunua simu lakini sina laini na sina kitambulisho. Jamaa akaniambia unataka kutumia laini gani nikamwambia vodacom, akaniambia vodacom na tigo ni pagumu hapo lazima uwe na kitambulisho cha taifa kwani ni mpaka uweke alama za vidole tena hata ukipoteza line au ikaharibika ukikumbuka namba na ukatupa namba za kitambulisho tunarejesha ndani ya dakika tano. Basi nikamwambia line ambayo ipo free ni zipi akaniambia Airtel na Halotel hizo unapata fasta. Nikamwambia nipe airtel. Akaweza kunipa. Akaniambia ndani ya masaa sita inabidi uweke hela ili uanze kutumia. Basi nikaweka elf moja nikaanza kutumia. Kesho yake nikamfuata anise halotel akanifanyia hivyo hivyo kama jana.


Kwa mrejesho huu ndio nikapata wasaa kuwa kumbe kisa cha matapel wa mitandao kuwa wengi hivi ni ruhusa ya mawakala wabovu wanaosajiri line lakini pia ni kutofatilia kwa wizara ya mawasiliano kupitia TCRA kuwabana Halotel na airtel kutumia alama za vidole na vitambulisho vya taifa halali. Kisa kikuu nikaja kuangalia makampuni mengi yanayojitangaza kuwa yanakopesha kwa muda mfupi na kuweka viwango fulani kutokana na mahitaji. Nikagundua malalamiko ya walioibiwa wengi wezi au matapeli walitumia Airtel na Halotel kufanikisha wizi. Makampuni ya Tala, Viva Mikopo Ltd, Kopa Fasta, Joketi Faundation, aircredit online. Mikopo ya Haraka Tanzania TCRA imeshindwa kufuatilia link za wanaojitangaza kuona kuwa ni kweli wanatoa huduma za haki au ni wezi. Nilipofuatilia Brela nikakuta kampuni nyingi hazipo kampuni nyingine zimefungiwa au zimeacha lakini matapeli wanazitumia kama zipo hai . Mfano kampuni ya Tala Tanzania. Kuna taperi anaitwa Dawson Bakena mwenye namba za usajiri wa airtel no. +255692913684 ametumika kuwatapel watu wengi sana na kesi nyingi zipo police lakini TCRA haikuwahi kumkamata hata baada ya watu kutoa taarifa nyeti. Wananchi waliotapeliwa wanashindwa kujua kama ana ushirika na vijana wa mtandao wa airtel au tu ni airtel hawajui. Kampuni ya Viva nayo inajidai ni wakala wa mikopo ya serikali lakini wakiombwa brela usajiri hauji kabisa japokuwa anatumia namba ya +255685250790 huyu anajinasibu kama wakala wa serikali kupatia watu mikopo jambo ambalo sio kweli.

Naomba Nape na Wizara , TCRA yake watoe majibu ni kwanini matapel wanatumia sana Airtel na Halotel? Kwanini TCRA haiwafungii kama wanakiuka mashart ya alama za vidole? Kwanini wanatumia mawakala wasio waaminifu kuandikisha line au wanataka kuvuna wateja kirahisi sana ambao ni hatari kwa taifa.
 
Back
Top Bottom