Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekutana na Wawakilishi wa Umoja wa Watoa Huduma za Matangazo kwa njia ya Waya (Cable Operators - TACOL), Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) na Baraza la Mashauriano la Watumiaji la TCRA (TCRA -CCC) katika kikao cha majadiliano kuhusu wizi wa maudhui na ukiukwaji wa hakimiliki.
Kikao hicho kilifunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Masuala ya KisektaDkt. Emmanuel Manasseh pamoja na Wadau wengine, leo tarehe 25/10/2021 katika Makao Makuu ya TCRA Jijini Dar es Salaam.