TCRA: Kuna tatizo la Mfumo wa Mawasiliano ya Intaneti kwenye Mkongo wa Baharini

TCRA: Kuna tatizo la Mfumo wa Mawasiliano ya Intaneti kwenye Mkongo wa Baharini

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kama umekosa huduma ya intaneti kwa saa kadhaa leo, tambua shida sio kifaa unachotumia bali ni tatizo la kiufundi lililotokea kwenye miundombinu ya intaneti iliyopitishwa baharini.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Jabir Bakari amelithibitisha hilo alipotafutwa na Mwananchi Digital leo Jumapili Mei 12, 2024.

"Kunaonekana kuna tatizo la kiufundi kidogo linalohusiana na 'marine cables' kwa hiyo tunajaribu kupata maelezo zaidi," amesema Dk Bakari.

Dk Bakari amesema kwa sasa wanaangalia namna ya kupata taarifa zaidi ili kujua ilipo changamoto ili kuchukua hatua.

Tatizo la mtandao wa intaneti limeanza tangu saa 4 asubuhi na hadi habari hii inapoandikwa saa 7.10 mchana huduma hiyo haijarejea.

===

Pia soma:
-
Kwa hii Shida ya Mitandao ya simu iliyotokea leo, turuhusu Starlink iingie Tanzania
- Mitandao ya simu ipige faida ya internet kwa mara ya mwisho. Elon Musk kuleta internet ya Starlink Tanzania
-
Watanzania wamefungiwa internet
 
Back
Top Bottom