TCRA: Mimi 'nimevote' kwa Jihan Dimachk, mshiriki wetu wa Miss Grand International, wewe je?

TCRA: Mimi 'nimevote' kwa Jihan Dimachk, mshiriki wetu wa Miss Grand International, wewe je?

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Piga kura kwa usalama! 👑✨

Unapomuunga mkono mshiriki wetu wa Miss Grand International, hakikisha unatumia viunganishi (links) rasmi pekee ili kupiga kura, na usitoe taarifa zako binafsi kama vile nywila au OTP

Screenshot 2026-10-06 at 18-56-01 Instagram.png
Screenshot 2026-10-06 at 18-56-20 Instagram.png
Screenshot 2026-10-06 at 18-56-42 Instagram.png

=====

Najiuliza hivi hii ndio kazi ya mamlaka hii? Nilidhani Wizara ya habari, Sanaa utamaduni na michezo ndio wangekuwa wanahamasisha kupigiwa kura kwa mrembwende huyu ila mambo yamekuwa tofauti kwani TCRA wameingia mzigoni kumnadi huku wakijificha kwenye kichaka cha Usalama wa kidigitali.

Najiuliza au ule mzigo wa pesa zinazopiga kura zinatoka serikalini kupitia kina Niffer ili jambo liwe kubwaa watu wajadili mamisi waache kujadili mambo ya haki nk.

Ila TCRA, kuhamasisha kupiga kura kwa mamilioni Jihan ashinde huku watoto wanakaa chini darasani na wagonjwa wanakosa dawa hospitali nao ni ukichaa.
 
Back
Top Bottom