TCRA mmeridhika na wizi wa vifurushi unaofanywa na Vodacom? Kifurushi Cha 1.2GB kinaisha less than 24hrs for normal chatting?

TCRA mmeridhika na wizi wa vifurushi unaofanywa na Vodacom? Kifurushi Cha 1.2GB kinaisha less than 24hrs for normal chatting?

Mkuu angalia balance kwanza hao jamaa wanatuma hizo message ili ujichanganye ununue kingine wakati bado una salio
 
Vifurush vinaisha fasta kiukweli sio mtandao huo tu,, ni mitandao yote, cjui wameset kitu gan
Kwa Halo tel hapana nitawatetea.

Baada ya kuona umumiani wa Voda na Airtel kwenye bundle, nimekuja kujibanza huku, pako shwari, ingawa nao mpaka upitie Halo- pesa kupata bundle la maana.
 
Makampuni ya simu Uhuru na mamlaka mnazojitwalia za kuwaibia wananchi kwa kutukomoa au kurejesha fedha za hasara mlizopata kipindi Cha nyuma si sahihi.

Nimejiunga kifurushi cha wiki 1.2GB cha Vodacom jana saa sita kasoro usiku. Then nikazima data hadi saa nne asubuhi. Nimewasha data since saa
MADELU kaharibu kabisa hii sekta, tutaimba haleluya hii miaka 4 ya samia
 
Mm nakuja na ushuhuda wa kuibiwa bando na TTCL
Kuna kile kifurushi chao cha Tsh elfu 10. Gb 10
Kwa siku 7
Ukishajiunga na iko kifurushi
Wanapunguza speed
hauwezi kuingia youtube wala kudownload chochote mtandao upo low kabisa
Wanabana hivyo karibu siku zote 7 kisha wanajifanya wao ni kama masungura fulani hivi
Siku ya mwisho wanarudisha ile speed ya kawaida ili wakutamanishe tena , unashangaa mtandao upo 4g plus + mwanzo mwisho,,
Ukija kutahamaki unaona alama ya >? Muda umeisha katikati ya utamu
Ukinunua tena kifurushi kipya umedinyea
Wanabinya tena speed ,,, ukiwasha data mtandao unakata kabisa mnara ,,
Juzi nikawatolea uvivu
Nikawatia mitusi wezi wakubwa nyie , mnawaibia wananchi kisha mnatangaza TTCL Imepata faida
Faida gani hiyo ya kutuibia
Nikaweka na namba yangu ya simu pale adharani katika page yao facebook
Wakaja wakaniomba radhi,,
Baada ya lisaa limoja nikaona mitandao upo full speed
Tangia juzi mbaka leo ttcl wameachia baada ya kubana kwa muda mrefu wananipiga tu mabando yangu,,
Ushauri usilalamike tu bila hoja na ushahidi
Nenda katika kurasa zao watie mitusi wataelewa tu… uwa wanafanya makusudi..
 
Makampuni ya simu Uhuru na mamlaka mnazojitwalia za kuwaibia wananchi kwa kutukomoa au kurejesha fedha za hasara mlizopata kipindi Cha nyuma si sahihi.

Nimejiunga kifurushi cha wiki 1.2GB cha Vodacom jana saa sita kasoro usiku. Then nikazima data hadi saa nne asubuhi. Nimewasha data since saa
SUJUI NDUGULILE NA TCRA WANAFANYA NINI KAMA WANSHINDWA KUTIHBITI KITU KIDOGO KAMA HIKI WANANCHI WANAUMIA WENYEWE WAPO NAANZA KUWAELEWA WATU WANAOSEMA WIZARA YA NDUGULILE IVUNJWE
 
Vodacom ni wapuuzi sana,
1. 1gb kwa 2000 per week. Then bando linaisha haraka mnooo
2. Sms za mwezi ni 2000tsh

Halotel
1. 1gb kwa buku tu per week, bado linadumu mnooo
2.Sms za mwezi ni 950 tsh ukinunua kwa halopesa.

Baada ya kuona ushenzi wanaoufanya voda nikaamua kuwapiga songesha ya 20000 na kutoa line yao. Mwezi wa pili sasa situmii voda. Niseme tu nimeipenda HALOTEL japo sometime internet yao inasua lakini ni bora, kuliko kuunga bundle la week kila siku.
 
Hao mbwa wa voda achana nao mkuu,nimehama mtandao wametenitia hasara mara kadhaa,huu wizi ulianza mwezi wa tano ukiwapogia wanakwambia ni kutokana na matumizi yako.

Hapo TCRA sijui wata track au itakuaje.Nafuu iko Tigo,halotel na Airtel japo internet zao zinasumbua.
 
Mkuu yote uliyoelezea ni sahihi, halafu hili janga si lako pekee bali ni la wote ila watu hawapigi tu kelele lakini maumivu wanayasikia kama si kuyaona!

Mie baada ya kuona hawarekebishi na waziri husika hana mpango, niling'oa hiyo line na kupachika Halo tel nikitumia voice na data.

Halo tel ingawa hawana kasi kama Voda, lakini hawana uhuni huo tena wana gharama nafuu kuliko Voda na pia ukiunga kifurushi cha data au voice kifurushi haki'expai' bali kina 'cease' na ukiunga kipya, kilicho cease kinasisimka na kusongeshwa kwa kuunganishwa na kipya ulichojiunga.
Si mhame mtandao? Mbona mm nimehama huko labda.kwa ajili ya sms na kupokelea simu tuu,Hawa jamaa wamefilosika sasa wanatapa tapa,hata kutumia miamala yao kwa sasa ni hatari sana.
 
"2. Ni kipi kimebadilika kabla ya utawala wa awamu iliyopita na utawala huu?"

Upuuzi wako uko hapo kwny hio statement,voda upigaji wa vifurushi wanafanya tangu miaka mingi iliyopita na mpk sasa kazi ya upigaji inaendelea vyema.
Mimi nime experience zaidi mwezi wa 5 baada ya kujiunga mara 2 ndani ya wiki na wiki haikuisha.

Walikuwa wanapiga ila kuanzia huo mwezi wamezidisha nikahama na mtandao.Wizi wa makampuni ya simu na mabenki wanatuibia Sana ila unatafuta kwenye nafuu.
 
Kumbe ndio wizi huu,mimi nimeshindwa kabisa kuelewa mara mbili nanunua kifurushi cha week Gb 1 lakini ndani ya 24hrs natumiwa sms umemaliza kifurushi chako,wakati huo mchana wote nimezima simu,sina Instagram,siangalii youtube,sidownload apps na files,natumia JF na Twitter tu.
vodacom acheni wizi[emoji53][emoji53]
Hahahaha unauziwa Gb ya kiini macho!
 
Vifurush vinaisha fasta kiukweli sio mtandao huo tu, ni mitandao yote, sijui wameset kitu gani.
Kwangu Tigo inakaa angalau saizi nataka niwe natumia Tigo na halotel kwenye bando Voda na Airtel nawatumia kwa. ajili ya mawasiliano ya kawaida
 
Kwangu Tigo inakaa angalau saizi nataka niwe natumia Tigo na halotel kwenye bando Voda na Airtel nawatumia kwa. ajili ya mawasiliano ya kawaida
Hahahah ni swala la muda tu! Vitaanza vichapo vya kibabe mpaka mtapoteana! Tigo ndio zao wakikimbiwa 😅😅😅
 
Back
Top Bottom