TCRA mmeridhika na wizi wa vifurushi unaofanywa na Vodacom? Kifurushi Cha 1.2GB kinaisha less than 24hrs for normal chatting?

Hahahah ni swala la muda tu! Vitaanza vichapo vya kibabe mpaka mtapoteana! Tigo ndio zao wakikimbiwa 😅😅😅
TTCL ipo mkuu yaani saizi nimelazimika kusajili line mitandao yote,kumiliki simu zaidi ya moja Ili kujihami ilimradi Bongo na Jf sihami haaaaa
 
Zantel wapo vizuri. Kwa uzoefu wangu zantel are clean. Vodacom wazee wa predatory business practice-hawkish ile mbaya. Worse vodavom seems to be beyond redemption.
Sasa nao si wa capitalise hii fursa? Hawana watu wa masoko kufanya ujasusi wa soko Ili watumie fursa?
 
I fill the pain baada ya bundle kuisha bila matarajio yako.
 
Mimi juzi wamemeza MBs 512 in less than 3 hrs. Sikuingia YouTube, wala siku download kitu chochote kile.

Yaan Voda ni wezi.
 
Jumamos iliyopita nimenunua kifurushi cha data cha 2,500 kufungua tu email kusoma natumiwa ujumbe kifurushi kimeisha. Hawa jamaa ni wizi wa mchana kweupe kabisa hawafai hata kidogo.
 
Mimi nimeishaga hama huko siku nyingi sana. Hakuna siku waliniudhi kama siku niliweka kifurushi cha GB 1 saa 4.30 usiku, nikawa nachat WhatsApp.. kufika saa 5 nikazima simu nikaweka kwenye chaji. Nimekuja kuwasha saa moja kamili, baada ya robo saa wananiambia MB zako zimeisha. Nikawahama hapohapo!!
 
Hili li mtandao majizi sana[emoji51]
 
Halotel bando linaisha kihalali kabisa..hao voda wezi Sana yaani mbs unaperuzi kidogo tu wanakutumia meseji umemaliza kifurushi chako
Hawa Sasa hivi laini yao nafanyia miamala tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…