TCRA mnajua usanii unaofanywa na DStv?

Mkuu, unaposema wanavuruga signal unakuwa una maana gani?, kwamba wana temper na dish lako au king'amuzi?.

Maana dish ndilo hupokea signals na kuzipeleka kwenye king'amuzi/decoder na kuwa decoded. Dstv wana uwezo wa ku update ving'amuzi vyao kupitia satellite na hufanya hivyo mara nyingi, ila hili la kucheza na signal ili wakulipishe ndo kwanza nalisikia kwako.

Nina miaka 9 sasa tangu noamze tumia dish lao, na sijawahi hata siku moja ita fundi wao kuwa dish/decoder imeleta shida. 9 solid years
 
Watu Masikini tuna taabu nyingi sana halafu kama ni Kipaji tulichonacho basi ni cha kupenda Kulalamika pasipo Kujiridhisha jambo fulani lenye Umuhimu na Utaratibu wake hasa Kibiashara.
 
Mkuu hapa nakupinga mimi ni shuhuda, walihamisha chaneli kwenye kifurushi cha juu
Mimi niliangalia mechi zote bila tatizo.
Mwanzo zilikuwa Chanel 224 lakini baadae walihamishia chanel 225
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…