TCRA mnajua usanii unaofanywa na DStv?

TCRA mnajua usanii unaofanywa na DStv?

Usanii huu wa DStv utaendelea mpaka lini?

Leo wameondoa channel namba 228 (super sport variety) Kwa vile Tu mashindano ya Olympic yataanza kesho kutwa!! Huu sio uungwana na ni wizi wa mchana tena ni usanii mtupu, haiwezekani tumelipia kifurushi ambacho hiyo channel inakuwepo halafu ghafla mnaondoa.

Kipindi cha mashindano ya Euro walifanya huu wizi Kwa watumiaji wa kifurushi cha bomba Kwa kuwaondolea channel namba 224, tunawaomba TCRA waangalie haya manyanyaso ya hawa DStv.

Inakuaje Media zingine hawana wizi kama huu WA DStv? Kwanini serikali wanashindwa kuwabana hawa makaburu ili waende sawa na media zingine?

Huu wizi wenu DStv ni kama mfano wa bus la kampuni Fulani ambalo walikuwa wakifikia Kwenye barabara ya lami wanatoza tena abiria kwasababu wapita Kwenye lami.
Haya ni majizi kama majizi mengine tu
 
...niko nje kidogo ya mada. Binafsi niliacha kutuimia dstv na kununua Azam maana nilishindwa kuangalia local channels za tz mfano ITV, star tv na kadhalika.
Na hadi Leo ukiniuliza kwanini hazipatikani sina jibu nnachokumbuka tu waliacha kuzionesha tangu kipindi kile Mwakyembe ni Waziri wa Habari, sasa hata kama Dstv walizinguana na baadhi ya hizi local channels labda kimaslahi inakuwaje hadi Leo hii hawajaweza kukaa na kuyamaliza!? na kuzirudisha Kama zamani!?
Nchi hii dah
 
Hao dstv Niliwaripoti TCRA kwa uhujumu waliofanya, kuondoa channel 224 bila taarifa na hivyo kunipunja kwa kunipa pungufu ya kile nilicholipia. Tarehe 16.07.2021 TCRA walitukutanisha mimi na DSTV kwa kikao cha usuluhishi pale Mawasiliano Tower. Mediation ilifeli, DSTV wakisema kuwa walitoa taarifa kuwa channel itahama hivyo hawakuwa na kosa lolote, mimi nikaendelea na msimamo wangu kuwa hakukuwa na taarifa za kuhama kwa channel, matangazo wanayoyasema yalikuwa ni ya vifurushi na sio uhamaji wa channel. Tumeambiwa bodi ya wakurugenzi wa TCRA watakapoketi kwa kikao, tutaitwa ili kusikilizwa suala letu na kutolewa uamuzi.

Mrejesho utafanywa humu. Tunachukua hatua.

[emoji23][emoji23][emoji119][emoji481]
 
IMG_6111.png
 
Dish la kawaida ya zamani Yale ,nashangaa watu wanahangaika! Kuna uzi humu wa unaelezea
Dish la kawaida yale ya futi sita au nane unaangalia nini, hata ukiwa unanunua decoder kila mara ili ku upgrade, bado baada ya mda zinakuwa scrambled. Useme labda kama sio mpenzi wa soka ndio utafaidi dish kubwa, otherwise hata cartoon za watoto wanazifunga.
 
Nimeagiza CANAL+ Zitakuja kama 100, zikifika nitawafahamisha wadau, hawa Dstv ni miyeyusho kinamna flani, CANAL gharama zake zipo chini mno, shida yake ni Lugha tu, lakini kwa wanamichezo hilo sio ishu lugha yetu ni moja
IMG-20220113-WA0005.jpg
 
Back
Top Bottom