Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Una hakika kuwa wanataka ajira yaani wanataka kuajiriwa....!!! Kama watakuwa wamepata kiinua mgongo kabla Hata hawajaanza kazi ya nini kusumbuka na mambo ya kuajiriwa....!!!Hao Mapacha iwe kweli au urongo hawataajirika popote
...Kiki, Wakati Mmoja anamminya mwenzake Mkono asiropoke kwenye TV ? Ingekuwa ni jambo la kupanga, angemminyia Nini mwenzake wakati wamepanga Kiki ?Hata kabla uchunguzi haujakamilika, critical analysis inabainisha hii ni kiki
...Saa hizi anajilaumu Kwa kuropoka ovyo...!Noma sana...Kuropoka ovyo nako sio poa.
Sahihi wamejimalizaHao Mapacha iwe kweli au urongo hawataajirika popote
Wazazi wao wamepoteza pesa bure kabisa kuwasomesha...Saa hizi anajilaumu Kwa kuropoka ovyo...!
Matatizo makubwa yapo kwenye misingi ya elimu yetu, mtu anasoma kwa lengo la kupata cheti tu na wala sio taaluma husika anayosomea.Hao ndio wasomi wetu wa sikuhizi. Hili Taifa sijui linaenda wapi aisee. Unafika mahali unajiuliza inawezekanaje msomi mzuri mwenye uelewa anaenda kwenye Media anaongea upumbavu kama huo akijua kabisa ukifanyika uchunguzi inaweza chuo husika kikatengua taaluma yake.
Walipangana waseme wamewahi kufanyiana mitihani lakini wssiende deep zaidi. Huyo mwenzake alikuwa anamzuia asiropoke sana....Kiki, Wakati Mmoja anamminya mwenzake Mkono asiropoke kwenye TV ? Ingekuwa ni jambo la kupanga, angemminyia Nini mwenzake wakati wamepanga Kiki ?
WOTE wachukuliwe Hatua !
Hapa ndipo kwenye tatizo. Ndio maana vijana wanaohitimu vyuo vikuu wana uelewa mdogo. Walikariri zaidi ya kuelewa.Matatizo makubwa yapo kwenye misingi ya elimu yetu, mtu anasoma kwa lengo la kupata cheti tu na wala sio taaluma husika anayosomea.
Hata muuliza swali naye ksuliza swali la kipumbavu sana. Haya sio maswali ya kuuliza.Hao ndio wasomi wetu wa sikuhizi. Hili Taifa sijui linaenda wapi aisee. Unafika mahali unajiuliza inawezekanaje msomi mzuri mwenye uelewa anaenda kwenye Media anaongea upumbavu kama huo akijua kabisa ukifanyika uchunguzi inaweza chuo husika kikatengua taaluma yake.
Umeweka assumption kibao bila fact.Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Kuna hiki kipande cha video kinachobamba mtandaoni kuhusu mapacha wawili ‘wanaokiri’ hadhrani kufanyiani mtihani ‘chuoni’.View attachment 2927982
Ukisikiliza kwa makini na kwa utulivu wa hali ya juu, utagundua kuwa hawa watu wanaigiza tu. Haiingii akilini watu wanaojua sheria za nchi kukiri hadharani kufanya uhalifu mkubwa kama huu huku wakifahamu kuwa wanatazamwa na dunia nzima na kwamba kufanya hivyo kunaweza kuwatia matatani kisheria.
Nina mashaka kwamba hii tamthlia itakuwa imepangwa na uongozi wa Wasafi TV ili kutafuta kiki uchwara ambazo pia zinaweza kuwaingiza hatiani ikiwa itabainika walifanya maigizo. Mashaka yangu yamegawanyika sehemu tatu:
Kwanza, mtangazaji Edo Kumwembe anauliza moja kwa moja kama mapacha hawa waliwahi kufanyiana mtihani, na wao wanakiri kweli waliwahi kufanyiana mtihani wakiwa ‘chuoni’. Na pia Edo amesema kufanyiana mtihani kunaweza kumuingiza mtu kwenye tatizo.
Hii inaashiria kuwa Edo anafahamu madhara ya watu kufanyiana mtihani ndio maana ametanguliza kauli ya kuingizana kwenye tatizo. Nafahamu Edo ni mwanahabari mwenye weledi wa hali ya juu na anayezingatia miiko ya utangazaji na utoaji habari. Hili lingekuwa sio igizo, kamwe asingethubutu kuuliza swali hili.
Pili, ukiendelea kusikiliza utasikia huyo mtangazaji aliye upande wa kulia (simfahamu jina) anasema kuwa huo ni uwongo na kuwa wataalamu wasisumbuke kwenda kufanya review (marejeo) kuhakikisha taarifa hii.
Tatu, wakati huyo pacha muongeaji (na ambaye anadai kumfanyia mwenzake mtihani) akijibu swali la Edo, pacha mwenzake anaonekana akimshika bega akiashiria kumkataza asiseme uongo hadharani. Huenda nafsi imemsuta mapema kabla mwenzake hajaongea lakini kwa kuwa huyo muongeaji huenda ndiye amepokea mpunga, anaamua kumpuuza na kuruka hewani.
Kwa mazingira haya, hii habari inaashiria moja kwa moja kuwa ni ya kutunga na imetangazwa hadharani ili kuwapa kiki Wsafi TV wapate watazamaji wengi kwenye mitandao yao ya kijamii, hasa Youtube, ili wapige pesa za kutosha kwa kujizolea watazamaji lukuki.
Turejee kwenye hicho ‘chuo’ ambacho mapacha wamesoma. Ukisikiliza kwa makini, hakuna mahali wametaja kuwa wamesoma Ardhi University. Kwa hiyo kitendo cha uongozi wa chuo kuibuka na hili tangazo wakati wakiwa bado hawajalifanyia kazi, nayo yawezekana ikawa kiki ya kutafuta kujulikana ili kuvutia wanafunzi kujiunga kwenye chuo hicho.
MAONI YANGU
Kwa taharuki hii waliyoisababisha Wasafi TV kwa lengo tu la kutafuta kiki uchwara, naomba TCRA iwafungie na kuwapiga faini ili liwe fundisho kwa vyombo vingine vya habari vyenye tabia kama hii. Wakifungiwa chaneli zao zote walau kwa miaka 5 na kupigwa faini kubwa watajifunza somo.
Aidha, kwa kitendo cha Ardhi University kuibuka kutoa matangazo wakati mapacha hawajawataja, naomba TCU iwapige faini kali, ikiwemo kumshusha cheo Makamu Mkuu wa chuo ili liwe fundisho kwa vyuo vingine vyenye tabia kama hii.
Nawasilisha.
Ni assumption kwa sababu hujaweka hata ushahidi wa wazi kuwa hawa wamepanga tu na si kwamba hao mapacha wamefanya hivyo (udanganyifu chuoni) kweli na kufunguka kwa kujisahau tu.Sio assumptions mkuu. Mbona hivyo ni vitu vinavyoonekana?