TCRA na Waziri Ndugulile, wanyonge mliotuumiza jana tunahitaji tu kupata majibu ya haya maswali yetu

TCRA na Waziri Ndugulile, wanyonge mliotuumiza jana tunahitaji tu kupata majibu ya haya maswali yetu

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
1. Baada ya Kuamuru jana kuwa Vifurushi vya zamani virejeshwe na viendelee je, ni Saa ngapi hilo litafanyika kwani mpaka sasa bado havijabadilika?

2. Je, wale ambao Jana walinunua Vifurushi vyenu vya Ukatili na Kutukomoa mtawasaidiaje na kuwafidia kutokana na Upuuzi wenu?

3. Ni saa ngapi Waziri Ndugulile na Mkurugenzi (Boss) Mkuu wa TCRA mtatangaza Kujiuzuru kwa Mateso ya Kimakusudi mliotupa Watanzania Wanyonge (Masikini) jana?

Ninayasubiri upesi sana tu Majibu yenu.
 
Hawawezi kutoa haraka hivyo.

Tamko linatoka warudishe vifurushi vya zamani wakati zile terms walizokubaliana hawajakaa mezani tena kuzitengua
Siasa bwana
 
Kifurushi cha voda cha 1000 SMS kwa mwezi kimekuwa 1500.

Hali ni mbaya sana kwa Tigo, Airtel na Halotel. Bora nibaki Voda tu maana huko kwingine hali inatisha sana.
 
Dah, jumba bovu linataka kumuangukia Faustine. Ila bado ana nafasi ya kujirekebisha.
 
Mtu aliye sahaulika kwa utendaji mbovu ni huyu Ndungulile

Nadhani Jumanne Mama amsaidie
Mh. Dr Faustine Ndugulile hajawahi kufanya jambo lolote la kuonekana katika Wizara yoyote aliyokuwa. Akiwa Wizara ya Afya huduma zilikuwa mbovu, watoa huduma ni miungu watu na wizi wa dawa kila mahali. Alikuwepo tu. Hana hata kimoja cha kuonesha alichosimamia.

Hata hii wizara mpya hatofanya lolote la maana zaidi ya kuharibu tu.
 
Mtu aliye sahaulika kwa utendaji mbovu ni huyu Ndungulile

Nadhani Jumanne Mama amsaidie
Nadhani si Ndungulile pekee, hawa mawaziri ndio walitoa miongozo na kusimamia sera mbovu za Meko. Kwa kuanzia Madam angevunja baraza lote.

Hata kama katiba ingekuwa haimlazimishi bado hekima ya kawaida inakataa, huwezi tumia mtu ambaye alikuwa sehemu ya tatizo kuleta suluhu.
 
Nadhani si Ndungulile pekee, hawa mawaziri ndio walitoa miongozo na kusimamia sera mbovu za Meko. Kwa kuanzia Madam angevunja baraza lote.

Hata kama katiba ingekuwa haimlazimishi bado hekima ya kawaida inakataa, huwezi tumia mtu ambaye alikuwa sehemu ya tatizo kuleta suluhu.
Kweli kabisa, unajua wao hawaguswi moja kwa moja na dhiki kama hizi, ndio maana wanaamua hata kutumia ushirikina na njia yoyote ile ili wapate nafasi ya uongozi.
 
Wanasema waziri sio lazima awe mtaalamu wa kada husika ya wizara yake, lakini huyu daktari wa binadamu anaonekana hajui anachokifanya huku kwenye mawasiliano.

Pia Madelu ajaribu kuangalia malalamiko ya watoa huduma za mitandao, wamekua ng'ombe mpole anayekamuliwa zaidi ya wenzake katika miaka mitano iliyopita.
 
1. Inashangaza sana, serikali inatoa tamko kusitisha bando jipya la data lakini mpaka sasa wanaendelea kukamua kwa rate mpya.
2. Hapo kuna hoja ya msingi, jana na leo watu wananunua kwa rate mpya inabidi wafidiwe.
3. Dhana ya kujiuzulu kwa watumishi wa umma ni mtihani, unaijua vieite wewe? Hawawezi kuacha kula shushu la vieite.
 
Back
Top Bottom