Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
TCRA NINAUNGANA KUWAOMBEA RADHI WASAFI TV.
Na Elius Ndabila
0768239284
Leo TCRA wametoa mvua ya miezi sita kwa Wasafi TV kwa kile kinachosemekana ni kurusha maudhui kinyume cha sheria.
Niwapongeze TCRA kwa kusimamia sheria hizi kwa uangalifu na nidhamu kubwa. Tunajua kuwa sheria ni msumeno, na hii inathibitishwa na adhabu hizi ambazo wamekuwa wakizitoa TCRA.
Nimejaribu kuiona ile picha ya huyo Msanii. Lakini sitaki kuzungumzia hii picha, nataka kuzungumzia hii adhabu.
Wasafi TV kupitia chombo chao hiki wameajiri watu wengi ambao maisha yao yanategemea pale. Kuwafungia miezi sita ni kuhatarisha maisha ya hawa watu. Lakini Wasafi Tv wanayomatangazo mbalimbali ya watu ambao wanakiamini chombo hicho kuwa ni munyororo tosha kwenye kuongeza wateja ktk biashara zao. Kuwafungia miezi sita ni kushusha biashara za watu ambako serikali inategemea kupata kodi.
Lakini ipo video inayoonyesha Wasafi Tv waliomba msamaha siku ileile. Sheria zetu zina option, ninaomba TCRA waangalie option nyingine ili kupunguza ukubwa wa adhabu hii ambayo imetokana na kosa la mpuuzi mmoja aliyeamua kuruhusu maudhui ambayo si sahihi kwa mjibu wa sheria zetu.
Ninaomba TCRA waangalie upya adhabu waliyotoa ili kuweza kuwasaidia watu hawa. Lakini pia ninashauri sheria zetu ziweze kutazamwa upya ili yanapotokea makosa kama haya aadhibiwe mtu na isiwe taasisi. Kwa mfano hapa angeadhibiwa huyu msanii na Wafanyakazi wa Wasafi TV ambao siku hiyo waliruhusu picha hizo kurushwa.
TCRA ni walezi, ninawaomba leo mvae sura ya ulezi ya kuonya, kushauri na kuhurumia. Picha hii imetudhalilisha wote, lakini ngoja tufanye exception kwa kumpa adhabu huyu Msanii na ikiwezekana kuwatoza faini ya fedha Wasafi TV na si kufungia chombo.