TCRA Taasisi ya umma inayowakandamiza wadau wake kwa makusudi

TCRA Taasisi ya umma inayowakandamiza wadau wake kwa makusudi

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,207
Reaction score
13,839
Kwanza nianze kwa kuliweka wazi, namfahamu jamaa yangu wa karibu aliyewekeza kwenye FM Radio.

Ni bora Mama Samia naye kalizungumzia tatizo la FEES a TCRA , tozo ambazo ni za juu mno bila sababu yoyote.

FEES za mwaka ni Dola $3,070 (na zaidi ya hapo kwa leseni ya kanda au Taifa) na ukichelewa kulipa interest ni 15%, sijui kama Benki Kuu inalifahamu hilo, maana TCRA si chombo cha fedha kutoza riba kubwa hivyo.

Leseni ikimaliza muda wake, kuhuisha leseni kila baada ya miaka mitano napo unalipa Dola $1,500 (na zaidi ya hapo kwa leseni ya kanda au Taifa).

Tunashukuru Mama Samia kaliongelea hili suala ambalo kimsingi naona lina wakomoa tu wawekezaji wa Kitanzania na kupunguza ajira kwa vijana.

Huko wenye kuanzisha TV ndio usiseme, leseni $15,000 na kuendelea.

Wabunge tunao lakini hawalisemei hili, utafikiri hawalijui.
 
Tmemsikia Mama Samia akililalamikia swala hili juzi akiongea na wahariri wa vyombo vya habari.

TCRA muwege na sura ya soni!
 
Tuna wabunge !wako wapi?hao si wabunge ni wachumia tumbo kama walivyo wengine.
 
Back
Top Bottom