TCRA tuambieni nani alimshitaki Polep[ole? Kuna matatizo makubwa ya maamuzi.

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,265
Reaction score
2,919
TCRA imemshitaki Polepole, Polepole akajitetea kwa TCRA, halafu TCRA ikamhukumu! That is no right! Kuna tatizo kubwa sana.

Muhusika amesoma kwa maringo sana juu ya mwenendo mzima wa maamuzi ya TCRA lakini mwishoni mtu unaona ni kama upuuzi wa aina fulani vile. Haijulikani makosa yameanzia kwa nani au chombo gani au taasisi gani. Yaani kuna mtu anaamua kusema una makosa, halafu utajitetea kwa nani sasa! Yaani TCRA ajione amekosea kwa Polepole!
 
Kwanini usijielimishe kwanza majukumu na mamlaka ya TCRA kabla ya kukurupuka kuwalaumu? Na serikali inapoyafungia magazeti huwa inasubiri mtu alete mashtaka, au awepo hakimu mwingine, au mtoa hukumu awe mwingine?

Mlipofurahia waliyopitia wabaya wenu zama za Mwendazake ndio nanyi mtapitia hayohayo nasi tutafuri wakati ninyi mnasononeka. Poleni 😊
 
Hiyo Haina tofauti na kesi ya Mbowe kwani aliyepeleleza ni polisi, aliyeshitaki ni polisi na shahidi ni polisi! Utawala wa ajabu Sana huu! Haya mambo nilidhani kuwa yalikwenda na mweñye awamu yake kumbe Bado yapo moto!
 
Hapa umempiga na kitu kizito.
 
Uzuri tulikuwa tunawaambia ubaya wa kutunga sheria za kikoloni wakadhani wanatungiwa wapinzani. Leo waliokuwa wanashangilia ndo waathirika.
 
Acha ujinga.
Mtoa leseni ni TCRA, Overseer ni TCRA, sasa unataka nani ajue makosa ya alopewa leseni kwa masharti ya TCRA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…