TCRA: Utapeli wa "Tuma kwa Namba Hii" umepungua sana nchini

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Akizungumza kupitia Power Breakfasta leo Oktoba 30, 2024, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma amesema "Kwenye utapeli kabla na baada ya zoezi la usajili wa laini za simu tofauti ipo kubwa sana. Ukiangalia ripoti ya Robo mwaka ya performance ya mawasiliano kwenye takwimu za mawasiliano inaonyesha takribani laini za simu zilizosajiliwa ni Mil. 80.

"Ukiangalia takwimu zinaonyesha katika ripoti ya September laini ambazo ziliripotiwa kuhusika na uhalifu na utapeli ni Elfu 16. Ukilinganisha na ripoti iliyopita ilikuwa ni laini Elfu 22.

"Ina maana kwa kadri wananchi wanavyoelimishwa endapo mtu atakutumia meseji tuma kwa namba hii, umeshinda bahati nasibu au kuna bonasi unatakiwa kupata. Au umepigiwa simu na mtu ambaye sio mtoa huduma akijaribu kupata taarifa zako ni lazima waripoti kwenye namba 15040.

"Ukiripoti zile namba zote ambazo zinakuja zinashughulikiwa na kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuzifungia"- Rolf Kibaja- Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na uhusiano kwa Umma TCRA.

CLOUDS MEDIA
 
Inasikitisha sana kuona watu wakitapeliwa kwa njia hii ya kishamba sana🤔
 
Inamaana mpaka Leo hawajapata source ya hiki?mbona kama hua wanashirikiana na watu wa kwenye hyo mitandao?
Maana namba zetu wanazipataje hasa ukisajili line mpya?
 
Akizungumza kupitia Power Breakfasta leo Oktoba 30, 2024, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma amesema "Kwenye utapeli kabla na baada ya zoezi la usajili wa laini za simu tofauti ipo kubwa sana. Ukiangalia ripoti ya Robo mwaka ya performance ya mawasiliano kwenye takwimu za mawasiliano inaonyesha takribani laini za simu zilizosajiliwa ni Mil. 80.

"Ukiangalia takwimu zinaonyesha katika ripoti ya September laini ambazo ziliripotiwa kuhusika na uhalifu na utapeli ni Elfu 16. Ukilinganisha na ripoti iliyopita ilikuwa ni laini Elfu 22.

"Ina maana kwa kadri wananchi wanavyoelimishwa endapo mtu atakutumia meseji tuma kwa namba hii, umeshinda bahati nasibu au kuna bonasi unatakiwa kupata. Au umepigiwa simu na mtu ambaye sio mtoa huduma akijaribu kupata taarifa zako ni lazima waripoti kwenye namba 15040.

"Ukiripoti zile namba zote ambazo zinakuja zinashughulikiwa na kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuzifungia"- Rolf Kibaja- Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na uhusiano kwa Umma TCRA.

CLOUDS MEDIA
Ninaheshimu takwimu zao, lakini bado kuna namba unakuta inakutumia ujumbe wa kitapeli leo, unairipoti na kuahidiwa itashughulikiwa lakini cha ajabu baada ya muda kama wiki mbili au mwezi kupitia hiyo hiyo namba unatumiwa ujumbe mwingine wa kitapeli tena.
 
Ni kweli hili tatizo linaweza kuwa limepungua lakini bado linaendelea licha ya kuongeza udhibiti kwenye usajili wa namba za simu. Swalli kama kuna udhibiti wa kutosha kwa nini bado utapeli huu unaendelea? Lazima kutakuwa na kasoro kwenye kampuni za simu au TCRA kwenyewe. Mwalimu Nyerere alisema: "It can be done, play your part".
 
Huo Utapeli umerudi kwa Kasi. Kwa siku napokea meseji tano
 
Wakukupigia waambie hapa imeingia pesa Mara tatu. Yakimakosa Ni ipi?
Watakata simu fasta
 
Yaani anaona ni sahihi kusema huo utapeli umepungua, badala ya kutuambia mkakati wa kuutokomeza kabisa!!

Kuna sababu gani sasa ya wananchi kusajili line za simu kwa alama za vidole kama mamlaka hazina uwezo wa kukabiliana na hao wahalifu wa kimtandao!
 
Akizungumza kupitia Power Breakfasta leo Oktoba 30, 2024, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma amesema "Kwenye utapeli kabla na baada ya zoezi la usajili wa laini za simu tofauti ipo kubwa sana. Ukiangalia ripoti ya Robo mwaka ya performance ya mawasiliano kwenye takwimu za mawasiliano inaonyesha takribani laini za simu zilizosajiliwa ni Mil. 80.

"Ukiangalia takwimu zinaonyesha katika ripoti ya September laini ambazo ziliripotiwa kuhusika na uhalifu na utapeli ni Elfu 16. Ukilinganisha na ripoti iliyopita ilikuwa ni laini Elfu 22.

"Ina maana kwa kadri wananchi wanavyoelimishwa endapo mtu atakutumia meseji tuma kwa namba hii, umeshinda bahati nasibu au kuna bonasi unatakiwa kupata. Au umepigiwa simu na mtu ambaye sio mtoa huduma akijaribu kupata taarifa zako ni lazima waripoti kwenye namba 15040.

"Ukiripoti zile namba zote ambazo zinakuja zinashughulikiwa na kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuzifungia"- Rolf Kibaja- Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na uhusiano kwa Umma TCRA.

CLOUDS MEDIA
Taarifa ya kusadikika ndani ya siasa, tulikuwa tunariloti lakini hatupati mrejesho wa hatua zilizochukuliwa, tumeamua kutoripoti.
 
Mimi nimepokea leo hii ujumbe huu kutokea

0738 819 679
Utanitumia kwa hîi TIGO 0675259049 j'ina ni LINUSI MALALO.
 
TCRA inasimamiwa na vichaa.walituhangaisha kusajili kadi Kwa kidole gumba Kwa kutudanganya utapeli utaisha kabisa lakini imekuwa kinyume chake na mnatuletea takwimu za kupikwa
 
Back
Top Bottom