TCRA waipa onyo wasafi Tv kwa kukashifu dini ya kikristo.

Sasa nabii halafu anamkashifu Yesu?? Au huko kwenye unabii anamhubiri Nani?? Maana unabii ni mojawapo ya karama za Roho mtakatifu ambaye huyo Roho mtakatifu tumeachiwa na Yesu (yoh14)ili awe msaidizi,mwalimu na mshauri katika safari ya kumjua Mungu.au ndo ile sikupendi Ila vitu vyako navipenda
 
Kama watu wanakesha humu kutetea matusi ya diamond katika nyimbo zake zilizojaa mashairi ya kwenda kwa mparange na kusafisha mitaro, sidhani kama hili litakemewa humu maana ni mazoea yaleyale!
 
Anahubiri utajiri

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu huyu shillah na masanja ni wachumia tumbo tu..
 
Unamzuwiaje mtu kuongea,ikiwa unamfanyia usaili(interview),halafu labda ni live!!?..kwa nini wanawaadhibu?
Wangekatiza kipindi na kuomba radhi hata kama ni live ila wao walishadidia ujinga wa huyo msengerema
 
Ingekuwa radio ya wakristu imefanya hivyo nadhani tungekuwa tunaongelea majivu maana wangekuwa waneshachoma moto
 
Hahahahaaaa

Kwanini serikali inaingilia?

Kwanini huyo Yesu asiende mahakamani kufungua shitaka kama kweli ameumia?

TCRA inaumia kwa niaba ya Yesu?

Muacheni huyo Yesu aliepata hayo maumivu ndio akashitaki
Ikiendelea hivi siku atatukanwa na Mudy ndio patachimbika si unawajua hawa ndugu zetu munkari wao ni kugusa tu.
 
Huyo Nabii amepewa adhabu gani na vyombo husika?

Maana Giggy Money alifungiwa kwa kuvaa alivyovaa
 
Alichoongea Shillah ni kweli, katika kundi la wahuni aliowataja Polepole "Mwana wa Mungu" hakosekani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…