TCRA wakomesha wizi wa kwenye mitandao tuma ujumbe kwenda namba 15040

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Endapo umetapeliwa au umetumiwa ujumbe wa utapeli, tuma ujumbe husika na namba ya aliyekutapeli au kukutumia ujumbe wa utapeli kwenda 15040. Huduma hii ni bure.

Tushirikiane kutokomeza utapeli kupitia simu za mikononi.

Sambaza ujumbe huu

cc @TCRA_Tz
@ConsumerCcc

Naishauri Tiisiiaraei wakate mzizi wa fitina kwa kuzuia meseji hizi zisisambazwe badala ya kutupatia sisi raia kazi ya kushughulika nao. Mantiki, matokeo na mafanikio ya kusajili laini za simu kwa alama vidole ni nini!?

Wezi wakiwa wajanja kuliko ninyi, afadhali jiuzuluni haraka muwapishe wataalam wa kazi. Awamu ya 5 inasifika kwa kutokomeza ujambazi wa manual ama hardcopy; sasa mambo yamehamia softcopy dijitali.
 
Shida ni kwamba zile namba zimwsajiliwa kwa majina innocent. Yaani hii issue inaelekea ina wengi so sio rahisi hivo eti umpate tu mtu kisa namba yake unayo. Utakuta iyo namba imesajiliwa na Mwalimu yupo Sengerema uko hajui ata kinachoendelea. Tatizo ni hawa Mawakala wasio na kichwa wala miguu.
 
Kama hakuna ajira utapeli lazima utamalaki ref: Nigeria au utetezi wa hushpuppy kwenye kesi yake.

Mfumo ulipo Tz hauwezi zuia utapeli. Hivi ni nani asajili line yake kwa alama za vidole kisha akafanyie utapeli? You guys (TCRA)mnatakiwa mfanye vitu beyond wanachofanya matapeli au matapeli wamewazidi elimu na akili? Tuwaajiri wao sasa.

Hizo namba mnazotaka mtumiwe mtaishia kuzifunga tu maana si za wahusika huku watu wakiendelea kutapeliwa kwa line mpya zinazosajiliwa tena.
 
Naishauri Tiisiiaraei wakate mzizi wa fitina kwa kuzuia meseji hizi zisisambazwe badala ya kutupatia sisi raia kazi ya kushughulika nao. Mantiki, matokeo na mafanikio ya kusajili laini za simu kwa alama vidole ni nini?

Wezi wakiwa wajanja kuliko ninyi, afadhali jiuzuluni haraka muwapishe wataalam wa kazi. Awamu ya 5 inasifika kwa kutokomeza ujambazi wa manual ama hardcopy; sasa mambo yamehamia softcopy dijitali.
Umezungumza jambo zuri sana, hili tatizo lipo kwenye Mamlaka nyingi.

PCCB wanakutaka ukiona mtu anatoa au kutaka rushwa uwaandikie barua badala ya kuitumia taarifa kuwakamata wahusika

NEMC nao wanataka kuandikiwa barua hata kama wao wanaona uchafuzi wa mazingira unaendelea

TCRA nao wanataka waambiwe, sielewi logic ya wao kutaka kuambiwa wakati mifumo yote imepita kwao, personally naafikiana nawe
kwamba hizi mamlaka zimekosa ubunifu, hao matapeli walitakiwa wawamalize wenyewe kimyakimya wangeacha
 
Hili ni jambo endelevu..

.
Screenshot_20210308-075909.png
 
Kwanini kila mtandao usiweke nambari na kuitangaza ya kutuma taarifa za matapeli?

Tunapokea meseji nyingi matangazo na mlolongo polisi huchukua muda mrefu sana. Nilitaraji kwa kutumia tehama, na uzuri wahusika wapo hewani maamlaka husika zingewakamata wahalifu kwa wakati.

2711100_Screenshot_20210310-091333.jpg
 
Hivi ni kweli ukituma wanawashughulikia!? Maana last week nilipigiwa simu na hao matapeli nikaambulia matusi tuu maana nilishawashtukia mapema nikaamua tuu niwamalizie dk,walivyokata simu yao nikawareport kwa hiyo namba ya tcra lakini sikupata any feedback kujua kuwa kweli wanalifanyia kazi jambo hilo au la..
 
Kama hakuna ajira utapeli lazima utamalaki ref: Nigeria au utetezi wa hushpuppy kwenye kesi yake.

Mfumo ulipo Tz hauwezi zuia utapeli. Hivi ni nani asajili line yake kwa alama za vidole kisha akafanyie utapeli? You guys (TCRA)mnatakiwa mfanye vitu beyond wanachofanya matapeli au matapeli wamewazidi elimu na akili? Tuwaajiri wao sasa.

Hizo namba mnazotaka mtumiwe mtaishia kuzifunga tu maana si za wahusika huku watu wakiendelea kutapeliwa kwa line mpya zinazosajiliwa tena.
Something is better than doing nothing.... Kama wakutumiwa hizo namba za matapeli na zile msg za Utapeli na wazifunga hizo namba immediately itasaidia huku wakiwatafuta wahusika.
 
Umezungumza jambo zuri sana, hili tatizo lipo kwenye Mamlaka nyingi.

PCCB wanakutaka ukiona mtu anatoa au kutaka rushwa uwaandikie barua badala ya kuitumia taarifa kuwakamata wahusika

NEMC nao wanataka kuandikiwa barua hata kama wao wanaona uchafuzi wa mazingira unaendelea

TCRA nao wanataka waambiwe, sielewi logic ya wao kutaka kuambiwa wakati mifumo yote imepita kwao, personally naafikiana nawe
kwamba hizi mamlaka zimekosa ubunifu, hao matapeli walitakiwa wawamalize wenyewe kimyakimya wangeacha
[emoji23] [emoji23] [emoji23] BAKWATA nao wanasubiri waandikiwe barua na Saudi Arabia...
 
Hivi ni kweli ukituma wanawashughulikia!? Maana last week nilipigiwa simu na hao matapeli nikaambulia matusi tuu maana nilishawashtukia mapema nikaamua tuu niwamalizie dk,walivyokata simu yao nikawareport kwa hiyo namba ya tcra lakini sikupata any feedback kujua kuwa kweli wanalifanyia kazi jambo hilo au la..
Ndiyo shida ya hizi mamlaka..
 
Endapo umetapeliwa au umetumiwa ujumbe wa utapeli, tuma ujumbe husika na namba ya aliyekutapeli au kukutumia ujumbe wa utapeli kwenda 15040. Huduma hii ni bure.

Tushirikiane kutokomeza utapeli kupitia simu za mikononi.

Sambaza ujumbe huu

cc @TCRA_Tz
@ConsumerCcc

View attachment 1719212

Hii heading nayo imekaa mkao wa kumwogopa Kiongozi Mkuu, eti "

TCRA wakomesha wizi wa kwenye mitandao tuma ujumbe kwenda namba 15040​

"Hebu watuambie nani wameshawahi kumkamata na nani wamemkomesha? Kila siku ngonjera mitandaoni, mambo ni yaleyale
 
Back
Top Bottom