Wale wa ndagu sio waganga ni matapeli.Hata za wale waganga wa kienyeji?
Umezungumza jambo zuri sana, hili tatizo lipo kwenye Mamlaka nyingi.Naishauri Tiisiiaraei wakate mzizi wa fitina kwa kuzuia meseji hizi zisisambazwe badala ya kutupatia sisi raia kazi ya kushughulika nao. Mantiki, matokeo na mafanikio ya kusajili laini za simu kwa alama vidole ni nini?
Wezi wakiwa wajanja kuliko ninyi, afadhali jiuzuluni haraka muwapishe wataalam wa kazi. Awamu ya 5 inasifika kwa kutokomeza ujambazi wa manual ama hardcopy; sasa mambo yamehamia softcopy dijitali.
Well saidYou guys (TCRA)mnatakiwa mfanye vitu beyond wanachofanya matapeli au matapeli wamewazidi elimu na akili?tuwaajiri wao sasa
Something is better than doing nothing.... Kama wakutumiwa hizo namba za matapeli na zile msg za Utapeli na wazifunga hizo namba immediately itasaidia huku wakiwatafuta wahusika.Kama hakuna ajira utapeli lazima utamalaki ref: Nigeria au utetezi wa hushpuppy kwenye kesi yake.
Mfumo ulipo Tz hauwezi zuia utapeli. Hivi ni nani asajili line yake kwa alama za vidole kisha akafanyie utapeli? You guys (TCRA)mnatakiwa mfanye vitu beyond wanachofanya matapeli au matapeli wamewazidi elimu na akili? Tuwaajiri wao sasa.
Hizo namba mnazotaka mtumiwe mtaishia kuzifunga tu maana si za wahusika huku watu wakiendelea kutapeliwa kwa line mpya zinazosajiliwa tena.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] BAKWATA nao wanasubiri waandikiwe barua na Saudi Arabia...Umezungumza jambo zuri sana, hili tatizo lipo kwenye Mamlaka nyingi.
PCCB wanakutaka ukiona mtu anatoa au kutaka rushwa uwaandikie barua badala ya kuitumia taarifa kuwakamata wahusika
NEMC nao wanataka kuandikiwa barua hata kama wao wanaona uchafuzi wa mazingira unaendelea
TCRA nao wanataka waambiwe, sielewi logic ya wao kutaka kuambiwa wakati mifumo yote imepita kwao, personally naafikiana nawe
kwamba hizi mamlaka zimekosa ubunifu, hao matapeli walitakiwa wawamalize wenyewe kimyakimya wangeacha
Ndiyo shida ya hizi mamlaka..Hivi ni kweli ukituma wanawashughulikia!? Maana last week nilipigiwa simu na hao matapeli nikaambulia matusi tuu maana nilishawashtukia mapema nikaamua tuu niwamalizie dk,walivyokata simu yao nikawareport kwa hiyo namba ya tcra lakini sikupata any feedback kujua kuwa kweli wanalifanyia kazi jambo hilo au la..
Hii heading nayo imekaa mkao wa kumwogopa Kiongozi Mkuu, eti "Endapo umetapeliwa au umetumiwa ujumbe wa utapeli, tuma ujumbe husika na namba ya aliyekutapeli au kukutumia ujumbe wa utapeli kwenda 15040. Huduma hii ni bure.
Tushirikiane kutokomeza utapeli kupitia simu za mikononi.
Sambaza ujumbe huu
cc @TCRA_Tz
@ConsumerCcc
View attachment 1719212
Mawakala gani? Na huwa wanashirikiana vipi?Safii ila tatizo matapeli yanashirikiana na mawakala!