TCRA Walimpongeza Nape Baada Ya Kutumbuliwa na Rais: Hii ni Dharau Kwa Mamlaka

Hili Shirika wanaanza na moja. Kavuruga mifumo yoote. Kwa manufaa ya Nani?. Anajua yeye.
 
Kitendo cha viongozi wa taasisi alizokuwa anaongoza Nape kutenguliwa eti kwa sababu wamempongeza aliekuwa bosi wao linaonyesha kuna tatizo kubwa serikalini.Haiwezekani mtu akatenguliwa halafu anaowaongoza wakamsifia !
Hapa alietengua inabidi atafakari kulikoni ???
 
Binafsi sikubaliani na kutenguliwa labda kwakuwa wamemsifia au kushukuru kwa utendaji wa boss wao,wangestahili onyo tu ingetosha kabisa.

Kwa hapa wenye mamlaka kwa maoni yangu wamefeli,,kwa maana nyingine wamekurupuka

Naamini kabisa wakitulia na kutafakar upya watajisuta,,,lau wamewatengua kwasababu za utendaji ni sahihi
 
Hizi ndio za hawa wanafiki. Ngoja itokee mtu kufichua utakuta nape kawapigia watu wake aliowahisani kufanya hili drama eti kushukuriwa na bodi na wakurugenzi. Na watawaponza wengi maana wajinga wenye kujiamini na wenye tamaa ya madaraka ni watu hatari. Hebu fikiri kile kisa cha nape akiwa na wadhifa huu huu anatimuliwa tena kuunda kamati kumchunguza mkuu wa mkoa makonda kitu ambacho hana madaraka nacho. Hebu ona pale nape akisema hadharani anamtetea wema sepetu kukutwa na madawa ya kulevya kwa kua baba zao walikua marafiki na mama zao wanatoka wote singida. Baada ya kutemwa kazi na jpm eti akataka kuitisha waandishi wa habari haijulikani kusema nini ila ni mtu mchochezi nje ya mamlaka. Yaani mama ajiandae kula matapishi maana hizi njema zitaleta ujinga dhidi yake lazima awadhibiti.
 
Drama ni nyingi sana.. Watu wamejishughulika nani katumbuliwa, kwa sababu gani... Wengine wamefurahia kwa sababu zao mbalimbali... Lakini cha msingi kwa haya yote, mwananchi wa kawaida anafaidika na haya mabadiliko.. Au ni sawa na mwalimu wangu zamani huko sekondari alisema.... hata yatokee mabadiliko gani, mwendesha mkokoteni atabakia vilevile..
 
Hizo pongezi hizo na hao wapongezaji ....sijui....kwa upepo ulivyo...?!!Yangu macho....Ila kwa vile ni tumbili tuuu...tunaweza tusijue hapa JF..
 
Suala la kufaidikaa hilo sahauu😀😀😀 jerry silaa ndo alikuwa anafaida direct kwa wananchi
 
Unadhani ile Tsh 300 Millioni ingetola wapi, ambayo Nape ameahidi kuchangia ujenzi wa soko la Bukoba kwa Mbunge Byabato, ambayo alisema ni hela ndogo.

Panapofuka moshi panaficha moto. Kimsingi DG TAKUKURU kama ana akili sawasawa inabidi leo awe ametuma vijana wake kwenye taasis zote zilizokuwa chini ya NAPE !!

Wataalamu wa Risk Management wanaita hiyo ni "red flag"
 
Kwahiyo hapo tayar mnamhukumu kwamba kuna sehemu kapiga hela,,acheni dhana,idhibitike ukwel uko wapi ndio muanze kutoa tuhuma
 
Wewe uliyeleta huu uzi, kwanini DG na BC wa TCRA wameachwa? wakati nao wamefanya hilo hilo lililopelekea wenzao wa TTCL, Posta UCSAF kuondolewa..
 
Safi sana mama
Ukiweza mtengue hata nyerere asiwe Baba wa taifa
 
Kwahiyo hapo tayar mnamhukumu kwamba kuna sehemu kapiga hela,,acheni dhana,idhibitike ukwel uko wapi ndio muanze kutoa tuhuma
Tuhuma lazima itolewa ili vyombo vya haki jinai vifanye kazi na kuthibitisha kuwa ni kweli au siyo kweli. Kama siyo kweli tuhuma inafutwa, kama ni kweli anaanza kusota na Mahakama

Huna haki ya kutuzuia kutuhumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…