Kusema ukweli kwa hili TCRA mnatuchanganya! Inaonesha hamjajipanga!
Usumbufu umekuwa mwingi mno!
- Tulisajili kwa majina mara ya kwanza, mkasema ni batili mkasema zoezi lirudiwe,
- Tukarudia tukasajili kwa vitambulisho vya kura, napo mkasema ni batili
- Mkasema tukamilishe usajili kwa kupiga picha mwaka juzi tukafanya hivyo lakini bado ikawa ni batili;
- Mwaka jana mkadai tusajili kwa vitambulisho vya NIDA kwa alama za vidole, tumefanya hivyo bado mnaona hiyo haitoshi!
- Mnataka mwaka huu wenye laini zaidi ya moja kwenye mtandao mmoja muwazimie simu zao walizozisajili
TCRA kwa hili sasa sio ungwana kabisa! Naona kama ni usumbufu mnaofanya wala siyo weledi!
Kuna majibu mepesi eti; kwa wamiliki wanaohitaji laini zaidi ya moja watatakiwa kusaini fom maaalum;
Swali!
- Kama electronic data za vidole hamziamini mtu amiliki laini apendavyo, je hizo fomu maalum ndo zitaaminika?
- Hizo fomu zinawafikiaje wananchi huko vijijini?
- Kuna wafanya biashara ambao wana office zaidi ya moja ambazo zinahitaji namba za simu zaidi ya moja hilo hamjalifikilia?
TCRA mtatukosea sana